1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rhodes afungwa miaka 18 kwa uvamizi wa bunge la Marekani

26 Mei 2023

Mwasisi wa kundi la mrengo mkali wa kulia la Oath Keepers nchini Marekani amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kwa tuhuma za kuchochea uvamizi kwenye bunge la nchi hiyo mnamo Januari 6, 2021.

USA Stewart Rhodes Gründer Oath Keepers
Picha: Jared Ramsdell/Journal Inquirer/AP/picture alliance

Hukumu hiyo ni kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa washitakiwa wa uvamizi huo.

Miongoni mwa washitakiwa 1,000, Stewart Rhodes alidaiwa kulielekeza kundi lake lililokuwa na silaha kwenda Washington na kufanya vurugu kwa lengo la kumzuia Joe Biden kuwa rais.

Jaji Amin Mehta alipokuwa akitangaza hukumu hiyo alisema njama za uchochezi ni miongoni mwa uhalifu mbaya zaidi ambao Mmarekani anaweza kuufanya.

Kamati ya Bunge la Marekani yatoa ripoti ya uvamizi wa Januari 6

Hukumu hiyo hata hivyo haikufikia malengo ya ombi la serikali la miaka 25, ingawa jaji Mehta alikubaliana na hoja juu ya mpango wa Oath Keepers, waliokuwa wakimuunga mkono aliyekuwa rais, Donald Trump, wa kufanya vurugu. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW