1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kiongozi wa zamani wa Bangladesh ahukumiwa miaka 10 jela

3 Februari 2026

Mahakama moja nchini Bangladesh imemuhukumu waziri mkuu wa zamani aliyepinduliwa kwa maandamano ya umma, Sheikh Hasina, kifungo cha miaka kumi jela kwa ufisadi wa ardhi.

Sheikh Hasina
Aliyekuwa waziri mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina, ambaye sasa amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa ufisadi akiwa uhamishoni India.Picha: Christophe Ena/AP Photo/picture alliance

Mpwa wa Hasina, Tulip Siddiq, ambaye ni mbunge nchini Uingereza kifungo cha miaka minne, kwenye kesi mbili za ufisadi unaohusiana na mradi wa ujenzi wa mji karibu na mji mkuu wa nchi hiyo, Dhaka.

Jaji Mohammed Rabiul Alam wa Korti Maalum aliwahukumu pia kifungo cha miaka saba wapwa wengine wawili, Azmina Siddiq na Radwan Mujib Siddiq kwa kuhusika kwao kwenye ufisadi huo.

Taasisi ya kupambana na ufisadi ya Bangladesh ilifunguwa kesi kwenye mahakama hiyo ikimtuhumu Hasina kushirikiana na maafisa wa serikali kujipatia viwanja sita vya nyumba kwa ajili yake na familia yake kwenye Mradi wa Mji Mpya wa Purchaba, licha ya kwamba hawakuwa na haki kisheria.

Hukumu hiyo imetolewa wakati serikali ya mpito inayoongozwa na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Muhammad Yunus, ikijitayarisha kwa uchaguzi mkuu hapo Februari 12, ambao chama cha Hasina, Awami League, kimezuiwa kushiriki. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW