Rais wa zamani wa Myanmar Win Myint aachiliwa huru
17 Aprili 2026
Matangazo
Taarifa iliyotolewa na televisheni ya taifa ya nchi hiyo imesema hatua hiyo ni sehemu ya msamaha uliotolewa na kiongozi wa Myanmar Aung Hlaing kwa jumla ya wafungwa 4,335. Myint alihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela kwa makosa mbalimbali yakiwemo uchochezi, udanganyifu wa uchaguzi na rushwa.
San Suu Kyi apunguziwa adhabu ya kifungo
Aidha kiongozi wa zamani Aung San Suu Kyi amepunguziwa pia kifungo cha miaka 27 anachoendelea kukitumikia. Suu Kyi alihukumiwa kwa makosa mbalimbali yakiwemo rushwa na uchochezi. Katika hatua nyingine Rais Min Aung Hlaing amebadilisha hukumu zote za kifo kuwa vifungo vingine katika msamaha alioutoa Ijumaa.