Kiongozi wa zamani wa wanamgambo Syria ashitakiwa Ujerumani
17 Mei 2024Kesi dhidi ya mwanamume mmoja raia wa Syria mwenye umri wa miaka 47 imeanza kusikizwa leo mjini Hamburg, kaskazini mwa Ujerumani kuhusiana na uwezekano wa kufanyika uhalifu wa kivita uliofanywa na wanamgambo walioiunga mkono serikali ya Syria kati ya mwaka 2012 na 2015.Maafisa wa zamani wa ujasusi wa Syria kushitakiwa Ujerumani
Msemaji wa mahakama kuu ya eneo la Hamburg, amesema mshtakiwa huyo aliingia Ujerumani mwezi Februari mwaka 2016 na kuzuiliwa katika mji wa kaskazini-magharibi wa Bremen mnamo Agosti 2 mwaka jana.
Idara ya mashtaka ya Ujerumani imemshtaki mwanamume huyo kwa makosa 21 ya uhalifu dhidi ya binadamu pamoja na uhalifu wa kivita.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa huyo alisema kuwa atatoa kauli yake kuhusu tuhuma hizo katika tarehe ya baadaye.Damascus.Kesi ya kijana wa Syria mzaliwa wa Ujerumani yaanza rasmi.
Kama mmoja wa viongozi wa kundi la wanamgambo la Shabiha wilayani al-Tadamon nchini Syria, mshtakiwa huyo anadaiwa kushiriki katika unyanyasaji wa raia pamoja na uporaji mali.