Kipaumbele ni kupunguza ukosefu wa ajira
23 Novemba 2007Matangazo
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesisitiza kuwa anadhamiria kuendelea na serikali ya mseto pamoja na Naibu mpya wa Kansela,Frank-Walter Steinmeier.Katika mahojiano mbali mbali,Merkel amesema anataka kutekeleza matakwa ya wapiga kura na kuongezea:
„Mkondo tulioanza nao umeinufaisha nchi.Na hiyo ni sababu ya kuamini kuwa serikali hii ya mseto,imefanya mema na itaendelea kufanya hivyo.“
Wakati huo huo,Kansela Merkel amesema,masuala yatakayopewa kipaumbele miaka miwili ijayo ni kupunguzwa kwa ukosefu wa ajira pamoja na kuimarisha utafiti na uangalizi wa watoto.