Wimbledon yaanza rasmi Jumatatu
1 Julai 2019Murray ambaye ni raia wa Scotland ana miaka 32 na anasema hatarajii mengi.
"Ningependa kufanya vyema nitakapokuwa uwanjani. Nacheza kwa ajili ya kupata ushindi na mimi ni mshindani sana. Lakini sijiambii kwamba, wiki nne au tano zilizopita nilikuwa sijui kama ningecheza hapa. Kwa hiyo sitarajii mengi. Lakini mara nitakapoingia uwanjani, nitajaribu kushinda kila mechi nitakayocheza," alisema Murray.
Wakati huo huo Mjapani Naomi Osaka ambaye alikuwa mchezaji nambari moja duniani upande wa kina dada anasema akili yake kwa sasa iko huru kutokana na shinikizo la kuitetea nafasi yake kama mchezaji nambari moja.
"Ndiyo, kisaikolojia kuwa nambari moja lilikuwa ni shinikizo kubwa sana kuliko nilivyotarajia. Kwa hiyo, ndio, nafikiri ni vyema kwangu kwa sasa kuorodheshwa wa pili hapa kwasababu jambo zuri ni kwamba ukishinda kipute hiki basi moja kwa moja unakuwa nambari moja. Kwa kweli hilo ndilo lengo langu kubwa. Sihitaji kufikiria kuhusu kuitetea nafasi yangu au kitu chochote," alisema Osaka.