Kirusi kipya cha Ebola chauwa 16 nchini Uganda
30 Novemba 2007Matangazo
Kirusi kipya cha ugonjwa wa Ebola wenye kusababisha maafa kimewaambukiza watu 51 na kuuwa 16 katika eneo moja la Uganda karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Dr.Sam Zaramba Mkurugenzi wa Huduma za Afya katika Wizara ya Afya nchini Uganda amesema kwenye taarifa kwamba mripuko wa ugonjwa huo huko Bundibugyo hivi sasa umethibitishwa kuwa ni Ebola.
Kirusi hicho kimeonekana kuwa sio kikali sana jambo ambalo sio la kawaida na waathirika wamekuwa hawavuji damu nyingi na wengi wao wamekufa kutokana na homa.