1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kisa cha Karadzic na Siemens.

30 Julai 2008

Kisa cha Karadzic na kashfa ya Siemens Ujerumani.

Aliekua Kiongozi wa waserbia wakati wa vita vya Bosnia,Radovan karadzic amewasilishwa leo mjini The Hague-Holland kukabili mashtaka ya kuhilikisha umma.

Gazeti la Schwäbische Zeitung laandika:

►◄

"kukabidhiwa karadzic Mhakama ya uhalifu ni mtihani mgumu ulioikabili serikali ya rais Boris Tadcic nchini Serbia.

Hatahivyo, kutiwa mbaroni kunakodaiwa sasa na Mahkama ya UM na Umoja wa Ulaya kwa mshirika wake Mladic,kunaweza kukasabaisha kuporomoka kwa serikali ya muungano ya Serbia.Marafiki zake wa chama-tawala katika serikali hiyo SPS watashughulikia mpasuko huo.

Na huo utakuwa mwisho wa haraka kabisa wa serikali ya Boris Tadic inayoelemea Umoja wa ulaya."

Gazeti la SÄCHSISCHE ZEITUNG likizungumzia mpango wa kuchangia Ujerumani ndege zake za kutoa maonyo na mapema-AWACS- kutumika nchini Afghanistan, laandika:

" Eneo la matumizi ya ndege hizo za Awacs huko Afghanistan halina vishindo vikubwa vya vita.Kwani, hata pale ilipoamuliwa kutumiwa picha za uchunguzi uliofanywa na ndege za Ujerumani za Tornados iliwekwa mipaka funali ili kuiridhisha Ujerumani.hii ni mipaka ambayo hailingani kabisa na ukweli wa mambo nchini Afghanistan.

Kutafautisha kati ya vikosi vyema vya Isaf na viovu vya OEF, daima hakukua sawa.Na tangu hali ya usalama nchini Afghanistan kuchafuka,si vibaya kuweka tofauti hiyo.Kwani, hata vikosi vya Isaf vinapigana hivi sasa na sio tu vinachimba visima nchini Afghanistan.Serikali ya Ujerumani katika taarifa zake siku za nyuma, haikuwa ikitoa picha halisi kuhusu mchango wa vikosi vya Ujerumani nchini Afghanistan.

Uamuzi wa kupeleka huko ndege za aina ya Awacs,kunaweza kukawa fursa ya kutambua hali hasa ya mambo ilivyo."

Likizungumzia mgomo wa sasa katika shirika la ndege la Ujerumani LUFTHANSA, gazeti la Neubrandenburg laandika:

" Mara hii mezani kuna swali :nani mwenye nguvu hapa: Nani aelewa kutetea bora zaidi masilahi ya wafanyikazi.

Chama cha wafanyikazi kinajikuta hivi sasa kikishindana na vyama vyengine -mfano wa chama cha UFO,kilichojitenga na shirika la vyama vya wafanyikazi la Ver.di.

Maonyo ya mabingwa wa maswali ya madai ya mishahara viwandani kuwa mashindano kati ya vyama vya wafanyikazi binafsi, kunaweza kukaongoza kutolewa madai ya mishahara kupita kiasi,sio hayana msingi.

THÜRINGER ALLGEMEINE lazungumzia ile kashfa ya rushua katika kampuni la Ujerumani la SIEMENS.

Laandika:

"Mahkama ilifikia hali ya kutojua ifanye nini tena:

Hapo Mei, mshtaki mkuu wa serikali mjini Münich, alisimamisha uchunguzi juu ya kashfa hiyo ya rushua katika kampuni la Siemens.Na sasa ni hofu inayotokana na kusimamia mkasa wa kuanguka kwa soko la hisa nchini Marekani na mashtaka yanayoweza kusababisha malipo ya mabilioni, ndiko kulikoifufua kesi hii.

Siemens inajaribu sasa kusonga mbele kukichunguza kisa hiki badala ya kukifunika..."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW