Kisiwa cha Lampedusa chashuhudia ongezeko la wahamiaji
15 Septemba 2023Kisiwa kidogo cha Lampedusa nchini Italia, kimetangaza jana kukabiliana na ongezeko la boti za wahamiaji wanaowasili kutoka Afrika Kaskazini baada ya idadi yao kufikia wahamiaji 7,000, sawa na wakaazi wote wa kisiwa hicho.
Kituo cha mapokezi kilichojengwa kuwahifadhi watu wasiozidi 400, kilizidiwa huku wanaume, wanawake na watoto wakilazimishwa kulala nje kwenye vitanda vya muda vya plastiki.Idadi ya wahamiaji waliokufa baharini yazidi 110
Mamlaka za kisiwa hicho zilitangaza hali ya dharura wakati ghasia zilipozuka siku ya Jumatano wakati wa usambazaji chakula na kusababisha polisi kuingilia kati.
Hapo jana wahamiaji zaidi waliwasili lakini wengi walihamishiwa kwenye maeneo mengine huku shirika la Msalaba Mwekundu la Italia likisema hali imedhibitiwa. Wahamiaji wengi hufikia kwanza kisiwani Lampedusa, kilichoko umbali wa karibu kilomita 145 kutoka pwani ya Tunisia.