JangaAfrika
Kisiwa cha Mayotte kukabiliwa na kimbunga kipya Jumamosi
11 Januari 2025Matangazo
Wakaazi wa kisiwa cha Mayotte wanajiandaa kwa dhoruba ya upepo mkali na mvua kubwa leo Jumamosi. Hii ikiwa ni chini ya mwezi mmoja baada ya kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi kuharibiwa vibaya na Kimbunga Chido.
Kisiwa cha Mayotte kimewekwa kwenye tahadhari ya hali ya hewa kabla ya kupita kwa Kimbunga "Dikeledi" kusini mwa eneo hilo. Mamlaka zilitoa wito kwa wakaazi "kuwa makini sana". Idara ya hali ya hewa ya Ufaransa ilitabiri "mvua kubwa na hali ya upepo", ikitarajia kuweko na mafuriko.
Mwezi uliopita, Kimbunga Chido kilisababisha uharibifu mkubwa, na kuua watu wasiopungua 39 na kujeruhi wengine zaidi ya 5,600 katika kisiwa hicho ambacho kinakaliwa na Ufaransa mashariki mwa Afrika.