1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KISMAYO: Mapigano mapya nchini Somalia

8 Mei 2005

Waziri mkuu wa Somalia amevunja ziara yake katika mji wa bandari wa Kismayo kusini mwa nchi kwa sababu ya machafuko mapya.Maafisa wamesema uhasama kati ya makundi ya wanamgambo umesababisha mapigano.Baadhi ya wanamgambo wameipinga ziara ya waziri mkuu Ali Gedi mjini Kismayo huku wengine wakiunga mkono.Hadi watu 14 walifariki katika mripuko uliotokea siku ya jumanne kwenye uwanja wa michezo mjini Mogadishu muda mfupi tu baada ya Gedi kuwahotubia wafuasi wake.Hii ni ziara ya kwanza kufanywa na Gedi nchini Somalia tangu kushika madaraka mwaka uliopita.Serikali ya mpito ipo Nairobi tangu kuundwa kwake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW