1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitengo cha kufuatilia amani Kongo kuanza kuhudumu Jumanne

5 Novemba 2024

Kitengo cha kufuatilia makubaliano ya kusitisha vita kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wanaoungwa mkono na Rwanda M23, kitazinduliwa rasmi Jumanne.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) Rais wa Angola Joao Lourenco (katikati) na Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (kulia) Felix Tshisekedi wakutana kwa mazungumzo juu ya vita nchini Kongo mnamo Julai 6t, 2022 mjini Luanda, Angola
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) Rais wa Angola Joao Lourenco (katikati) na Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo (kulia) Felix TshisekediPicha: JORGE NSIMBA/AFP

Siku ya Ijumaa, Angola ilisema kuwa itaongoza kitengo hicho cha kufuatilia mkataba wa kusitisha mapigano Kongo kitakachowajumuisha maafisa wa Kongo na Rwanda.

Waasi wa M23 wameteka maeneo kadhaa mashariki mwa Kongo

Waasi hao wa M23 wengi wao kutoka kabila la Watutsi, wameteka maeneo kadhaa ya mashariki mwa Kongo inayokabiliwa na ghasia tangu mwaka 2021 na kuwalazimu maelfu ya watu kukimbia makazi yao na pia kusababisha mzozo wa kibinadamu.

Angola yaituhumu M23 kwa kukiuka usitishaji mapigano Kongo

Makubaliano ya kusitisha mapigano yaliotiwa saini mwezi Agosti yalileta utulivu katika uwanja wa vita, lakini tangu mwishoni mwa mwezi Oktoba, kundi hilo la M23, limekuwa likifanya mashambulizi katika jimbo la Kivu Kaskazini kuelekea katika mji wa kimkakati wa Pinga.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW