Kitisho cha bomu chafunga shule Ufaransa
16 Oktoba 2023Matangazo
Hayo yametokea katika shule ambayo mwalimu mmoja aliuawa kwa kuchomwa kisu wiki iliyopita katika shambulizi linaloaminika kuwa lilitendwa na wafuasi wa itikadi kali za kidini.
Mamia ya wafanyakazi na wanafunzi wameondoka katika shule hiyo, huku Rais Emmanuel Macron akikatiza mipango ya safari zake nje ya nchi siku ya Jumatatu (Oktoba 15) ili kuandaa mkutano wa usalama.
Soma zaidi: Polisi wafanya msako baada ya kitisho cha bomu Ufaransa
Mamlaka ya mkoa wa Pas-de-Calais imesema kuwa hatua zote za tahadhari na kiusalama zimechukuliwa.
Kufuatia tukio hilo la mwalimu kuchomwa kisu, Ufaransa iko katika hali ya tahadhari dhidi ya vitisho vinavyohofiwa kupangwa na magaidi.