UgaidiMali
Kitisho cha ugaidi ni kikubwa Afrika, Afghanistan na Ulaya
2 Februari 2024Matangazo
Ripoti hiyo pia imebainisha ongezeko la ugaidi katika kanda nyingine ikiwa ni pamoja na Ulaya hasa kufuatia mashambulizi ya mwishoni mwa mwaka jana nchini Ufaransa na Ubelgiji.
Jopo la wataalam limesema katika ripoti hiyo yenye kurasa 23 kwamba utawala wa Taliban nchini Afghanistan bado una uhusiano wa karibu na kundi la Al-Qaeda.
Kanda ya Afrika Magharibi na Sahel pia imeshuhudia ongezeko la vurugu na vitisho huku serikali ya Somalia ikiendeleza mashambulizi dhidi ya kundi la Al-Shabaab ambalo bado lina nguvu.