1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kitisho cha usalama chatanuka mashariki ya kati

30 Julai 2026

Shambulio dhidi ya meli mbili za kusafirisha gesi katika bandari ya Damietta Misri lazusha wasiwasi zaidi wa kiusalama Mashariki ya kati

Mfereji wa Suez nchini Misri ndio njia pekee salama iliyobaki kwa usafirishaji mafuta ya Saudi Arabia
Mfereji wa Suez nchini Misri ndio njia pekee salama iliyobaki kwa usafirishaji mafuta ya Saudi ArabiaPicha: Ahmed Gomaa/Xinhua/picture alliance

Shambulio la droni lililozilenga meli za kusafirisha gesi katika bandari ya Damietta kwenye bahari ya mediterrania nchini Misri limetajwa kuwa ishara inayoonesha uwezekano wa vita vya Marekani na Iran kuenea kwenye maeneo mapya.

Shambulio hilo limeibuwa kitisho katika usafiri wa meli kupitia mfereji wa Suez,ambao ni njia ya mwisho salama iliyobakia ya kusafirisha mafuta ya Saudi Arabia. Waasi wa Houthi wadai kuishambulia meli ya Kigiriki

Baraza la mawaziri la Misri limesema hivi leo kwamba uchunguzi wa awali umeonesha droni ambayo haikutambuliwa ilisababisha mripuko wa moto baada ya kuzishambulia meli mbili katika bandari ya Damietta.Vyanzo vyenye ufahamu wa suala hilo vimeeleza kwamba moja ya meli zilizoshambuliwa inamilikiwa na Marekani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW