Kitisho kwa watoto Somalia
20 Julai 2011Matangazo
Ripoti ya shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu, Amnesty International, imeyasema hayo mapema hii leo.
Kundi hilo lililo na makao yake mjini London Uingereza, limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kulinda haki za watoto katika nchi hiyo iliogawanyika kivita, ambapo maelfu ya watu wanakimbia ukame mkubwa.
Umoja wa mataifa hapo jana ulitangaza kuwa kiasi ya wasomali 4000 wanakimbia nchi hiyo kila siku wakati Ukame na baa la njaa umesababisha vifo vya watu zaidi ya 7 kila siku kutoka kila wakaazi 10,000.
Huku idadi kubwa ya vifo, ikiwa ni ya watoto walio na umri wa chini ya miaka 5.
Mwandishi: Maryam Abdalla/dpa, afp, reuters
Mhariri:Hamidou,Oummilkheir