1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kituo kingine cha forodha katika mpaka wa Kenya na Uganda

Michael Kwena1 Oktoba 2021

Kenya na Uganda zimekubaliana kuongeza kituo kingine cha forodha katika mpaka wake ili kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kati ya mataifa hayo.

Afrika Grenzübergang Stau LKW Kenia Uganda
Picha: Brian Ongoro/picture alliance

Kuidhinishwa kwa ujenzi wa kituo kingine cha forodha kwenye mpaka wa kenya na Uganda,kunatarajiwa kupunguza misongamano ya matrela ya mizigo ambayo huchukuwa muda mrefu kukaguliwa kutokana na kuwepo kwa vituo viwili pekee vya forodha vikiwa ni vituo vya busia na Malaba.

Kwa mujibu wa serikali za kenya na Uganda,kujengwa kwa kituo kingine cha forodha eneo la Muluanda,kutasaidia kuimarisha uchukuzi baina ya mataifa hayo mawili.

Akizungumza  walipozuru sehemu iliyopendekezwa kujengwa kituo hicho,naibu gavana wa Busia Moses Mulomi,ametaja forodha zilizoko kwenye mpaka wa kenya na Uganda kwa sasa kama inayochangia asili mia kubwa ya uchumi kwa taifa

"Hii itaimarisha uhusiano kati ya wakaazi na pia ubadilishanaji wa bidhaa kati yao.tunashirikiana kwa mambo mengi sana.Kwa sasa,asili mia 43 ya bidhaa tunazouza nje ya nchi zinapitia kwenye forodha za aidha Busia au Malaba kuelekea Uganda na mataifa mengine ya afrika kama vile congo na hata sudan kusini”, alisema Mulomi.

Hata hivyo,ujumbe kutoka Uganda umeomba muda zaidi kujadiliana na wizara husika kuhusu ukubwa wa ardhi itakayotumika kwenye mradi huo.

Soma pia:Kenya, Uganda kushiriki mazungumzo kuhusu mvutano mpakani

Hatua  ya kupunguza misongamano mpakani

Picha: Getty Images/AFP/B. Ongoro

Ujumbe huo ulioongozwa na Meja Martha Asiimwe umepongeza mahusiano yaliyopo kwa sasa baina ya kenya na Uganda.Ujenzi wa kituo cha forodha cha Muluanda na kile cha Bunyide upande wa Uganda,kutapunguza msongamano ambao hushuhudiwa kwenye forodha zilizopo kwa sasa.

"Tunaomba kwa heshima kwamba,mturuhusu kwa muda Fulani ili tuwashirikishe wakaazi na wizara husika namna mlivyofanya kisha tutaleta ujumbe ambao tutakuwa tumepewa”,alisema Asiimwe.

Wakati huohuo,wakaazi kutoka Muluanda wametaja ujenzi wa kituo cha forodha kama kitakachotoa nafasi zaidi za ajira kwa wakaazi Pamoja na kwamba kitarahisisha shuguli za kibiashara kati ya kenya na Uganda.

Soma pia:Malori yaliyobeba mahindi yakwama mpakani Namanga 

Matararajio ya wakaazi 

Huyu hapa ni mmoja ya wakaazi wa Muluanda:

"Kituo hiki kitasaidia kupunguza msongamano mjini busia na Malaba na pia kaunti ya busia itapata ushuru.Vijana hapa watapata ajira,na akina mama watafanya bisahara na eneo litabadilika kiuchui kabisa.”

Ujenzi wa kituo kingine cha forodha mpakani busia ulikuwa umeidhinishwa na rais mstaafu Mwai Kibaki mwaka wa 2009.

Kwa sasa,mpaka wa kenya na Uganda hutumia vituo viwili vya forodha vikiwa ni ile ya Busia na Malaba.