1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

 Kiungo wa Woflsburg Yannick ajehuriwa usoni

Josephat Charo
11 Mei 2020

Jeraha la Yannick ni pigo kubwa kwa Wolfsburg wakati timu hiyo ikijiandaa kujiimarisha Bundesliga itakapoanza tena Mei 16.

Fußball 1. FC Union Berlin - VfL Wolfsburg Yannick Gerhardt
Picha: picture-alliance/dpa/A. Gora

Kiungo wa Wolfsburg Yannick Gerhardt amepata jeraha baya usoni baada ya kugongana kichwa na mchezaji mwenzake na kupasuka wakati wa mazoezi. Jeraha hilo lilitokea wakati wa mechi ya mazoezi ya vikosi viwili vya wachezaji 11 kwa 11.

Kocha Oliver Glasner alisena Jumapili (10.05.2020) katika mkutano wa waandishi wa habari kwa njia ya video kwamba kujeruhiwa kwa Gerhardt ni pigo kubwa kwa klabu hiyo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 amelazwa hospitali na lazima afanyiwe upasuaji.

Wolfsburg inaanza tena Bundesliga wakiwa na miadi na Augsburg Jumamosi ijayo.

Madaktari wa vilabu vya Ujerumani walionya awali kwamba huenda kukatokea ongezeko la majeraha kufuatia miezi miwili ya ligi kusimama.

(dpa)

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW