1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kivu Kaskazini yakabiliwa na mlipuko wa homa ya nyani

25 Juni 2024

Mkoa wa Kivu Kaskazini kwa sasa unakabiliwa na mlipuko mbaya wa ugonjwa wa Monkeypox, ugonjwa wa virusi vya kuambukiza na unaoweza kuwa hatari kwa afya ya umma.

Ugonjwa wa homa ya nyani
Mtu anayeugua ugonjwa wa homa ya nyaniPicha: Arlette Bashizi /REUTERS

Waziri wa Masuala ya Kijamii wa Kivu Kaskazini, Prisca Luanda Kamala, amesema katika taarifa yake kuwa. 

"Wananchi wapendwa wa Kivu Kaskazini, serikali ya mkoa wa Kivu Kaskazini inawatangazia kuwa kuna kisa cha ugonjwa wa Monkeypox au ndui ya nyani ambacho kimethibitishwa katika eneo la afya la Karisimbi mjini Goma. Hadi sasa, visa vinane vimeripotiwa. Ugonjwa huu ni hatari sana na unaambukiza sana. Uwepo wa visa hivi katika mji wa Goma na maeneo jirani ni tishio kubwa na hatari kubwa ya maambukizi kwa wakazi wote wa mji wa Goma.

Mtu anayeugua virusi vya homa ya nyaniPicha: Gemeinfrei/CDC's Public Health Image Library

Ugonjwa wa Homa ya nyani au Monkeypoxunasababishwa na virusi vya aina ile ile ya ndui na unaenea hasa kwa njia ya mawasiliano ya moja kwa moja na wanyama walioambukizwa, hususan panya, pamoja na maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda kwa binadamu. Dalili ni pamoja na homa, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, ikifuatiwa na kutokea kwa vipele vya ngozi ambavyo vinaweza kuenea mwili mzima.

Visa vya homa ya nyani vyaongezeka mara tatu barani Ulaya

Wakazi wa mji wa Goma wako katika hali ya kukata tamaa na hofu. Wanaogopa kuenea haraka kwa ugonjwa huu, ambao unaweza kusababisha vifo vya watu wengi, hasa kwa kuwa mji wa Goma tayari umejaa mara tatu na wakazi waliohamishwa. Sikiliza hapa maoni ya baadhi ya wakazi wa Goma:

"Nina wasiwasi sana. Goma ni mji ambao tayari umejaa, hili ni tatizo kubwa sana. Kama leo tunayo Monkeypox, hatari ya maambukizi ni kubwa sana."

 "Kwa kweli ugonjwa huu unanitia hofu. Hatujui jinsi ya kujilinda. Najiuliza nini kitatokea kwa wananchi wenzetu walio katika kambi za wakimbizi. Ugonjwa huu unatupa hofu kubwa."

Chanjo ya ugonjwa wa Homa ya Nyani imepatikana

00:49

This browser does not support the video element.

Mtu mmoja afariki dunia kufuatia homa ya nyani Afrika Kusini

Daktari Arnaud Masirikia Muhigirwa anasema kuwa wakazi wa mji wa Goma wanapaswa kutulia na kufuata hatua za usafi pamoja na kuvaa barakoa, kwa sababu kuenea kwa ndui ya nyani ni mchanganyiko kati ya ugonjwa wa virusi vya Ebola na Covid-19.

"Kile ambacho wakazi wanapaswa kufanya ili kujilinda dhidi ya ugonjwa huu ni kuepuka mawasiliano ya moja kwa moja na kufuata sheria za usafi. Pia kuna chanjo ambayo itakuja baadae. Kwa hiyo, ni muhimu kwa wakazi kubaki watulivu."

Aidha, mamlaka za afya za Kivu Kaskazini zinafanya kazi ya kutambua na kutenga haraka visa vinavyoshukiwa, kufuatilia mawasiliano ya karibu ya wagonjwa waliothibitishwa, na kuweka mpango wa chanjo ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa huu.

Jamhuri ya Kongo yaripoti visa kadhaa vya homa ya nyani, mpox

Ugonjwa huu ulioanza kugunduliwa nchini Denmark mwaka 1958, tayari umesababisha vifo karibu 300 tangu mwanzo wa mwaka huu, nchini DRC.

 

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW