1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kivumbi chatazamiwa katika mkutano mkuu wa ANC

Jane Nyingi
28 Juni 2017

Nchini  Africa Kusini  hasira zinaongezeka ndani ya  chama tawala cha  African National Congress. Haya yanajitokeza wakati chama hicho kikijiandaa  kwa mkutano wake mkuu tarehe 30 Juni  hadi  Julai 5.

Südafrika Zuma hält Rede im Orlando Stadion in Soweto
Picha: Getty Images/AFP/M. Safodien

Chama cha ANC kitaanza mkutano wake Ijumaa ya hapo kesho  kujadili mwelekeo wa chama mkutano ambao unategemewa kuendelea kugubikwa na mivutano ya ndani kuhusiana . Chama hicho cha ANC kimeshuhudia kashfa chungu nzima za rushwa zinazomuandamana rais Jacob Zuma.Yamekuwa yakifanyika maandamano nchini Afrika Kusini kumshinikiza rais Zuma aliyepoteza umaarufu kujiuzulu. Yote hayo  yamekuwa yakifanywa na upinzani unaodai rais Zuma amepoteza uhalali, na huku nazo kura za kutokuwa na imani nae zikigonga mwamba  bungeni.Pamoja na hayo wasiwasi  wa kuwepo mivutano zaidi ndani ya chama hicho tawala umeongezeka huku pia  umaarufu wa chama hicho ukizidi kuporomoka.

Wasiwasi waendelea ndani ya ANC

Chama hicho kinafanya mkutano wake huo wa kisiasa  siku ya ijumaa kikiwa katika mazingira hayo ya wasiwasi.Wajumbe elfu tatu watashiriki kikao hicho  kitakacho endelea kwa siku tano kujadiliana  kuhusu mwelekeo wa chama hicho. Ajenda kuu zitakazo jadiliwa na  wajumbe hao zitajikita hasa katika maswala yanayohusu mageuzi kwenye mpango wa kijamii na uchumi. Ukosefu wa ajira nchini Afrika Kusini umefikia asilimia 27.7 ikiwa ni kiwango kikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa huku pia hali ya kiuchumi katika robo ya kwanza ya mwakaikiwa imeporomoka kwa 0.7 asilimia.Kwa maneno mengine taifa hilo la Afrika Kusini limeshaingia katika mporomoko wa kiuchumi.Sambamba na hayo chama cha ANC kimeshapoteza misingi yake na juu ya hilo  hata imani ya wananchi inazidi kupungua. Hii imetokana  na hali iliyoshuhudiwa kwenye matokeo ya uchaguzi pamoja na kukosolewa waziwazi chama hicho amesema  Jeff Rabete ambae ni waziri katika ofisi ya rais kabla ya mkutano huo. Viongozi kama Rabete wanahisi mjadala kuhusu rais Zuma unaonyesha ni jinsi gani chama hicho kinavyozidi kugawika.Mkutano huo kwa hakika unataka kutafuta njia ya kukiunganisha. Chama hicho, kilichoongoza  mapmbano ya ukombozi dhidi ya sera  ya kibaguzi Apartheid, i kinataka kutumia swala la kufanyika mageuzi ya kiuchumi kuwavutia wapiga kura zaidi  katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2019.Na hapo rais Zuma atakuwa amefikia mwisho wa muhula wake wa pili madarakani.Mkutano huo  mkuu kwa mujibu wa wachambuzi kama Daniel Silke  ndio utakaotoa sura halisi  ya maamuzi yatakayofanyika katika mkutano mkuu wa chama mwezi Desemba kuhusu nani atakiongoza chama hicho baada ya Zuma. Mchambuzi huyo akizunguma za DW amesema mkutano huo pia utatoa mwelekeo kuhusu mpango mzima wa chama hicho ikiwa kitafwata mkondo wa kizalendo na siasa kali au kunyamaziana zaidi na kuwepo uwazi.Tayari ilani ya ANC inaonyesha  kutaka kupendelewa zaidi kwa waafrika weusi. Hata hivyo Makamu wa rais  Cyril Ramaphosa ameonekana  kulizungumzia swala hilo kwa uwangalifu akisema ni bora misingi ya uwazi izingatiwa kama inavyoelezwa katika ilani inayohusiana na swala zima la uhuru.

Rais Jacob ZumaPicha: Imago/Gallo Images
Maandamano ya kumshinikiza rais Zuma kujiuzuluPicha: Reuters/S. Sibeko

Ikumbukwe kwamba rais Jacob Zuma  amekuwa akikosolewa sana  kuhusiana na  kashfa za rushwa pamoja na uhusiano wake na familia tajiri na maarufu ya kihindi ya Ghupa,na kwa maana hiyo basi mchambuzi Daniel Silke anasema chama hicho cha ANC kinatarajia   baada ya  Zuma kuondoka  itakirudishia heshima na imani  miongoni mwa wafuasi wake na wapiga kura. 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW