UchumiAfrika
Kiwanda cha mafuta cha Dangote chaanza uzalishaji Nigeria
13 Januari 2024Matangazo
Kiwanda kikubwa kabisa Afrika cha kuchakata dizeli na mafuta ya ndege kilichojengwa na tajiri mkubwa kabisa barani humo kimeanza kufanya kazi.
Kiwanda cha Dangote chenye uwezo wa kuzalisha mapipa 650,000 kwa siku huenda kikaleta mapinduzi wakati kitakapoanza kufanya kazi kikamilifu kwa kusaidia kukomesha utegemezi wa Nigeria wa kuagiza mafuta kutoka nje.
Kampuni hiyo imesema leo ni siku kubwa kwa Nigeria. Kiwanda hicho kikubwa kilichocheleweshwa ambacho kilijengwa na bilionea wa Nigeria Aliko Dangote kimesema kinatumai kuwa bidhaa take zitaanza kuuzwa mwezi huu, lakini haijafahamika ni lini kiwanda hicho kitaanza uzalishaji kamili au kuanza kuchakata mafuta ya petroli.