Kizazi kipya cha makundi ya itikadi kali Nigeria
15 Machi 2022Baadhi ya wataalamu na wachambuzi wa mashambuli ya wanajihadi wanasema kuwa kizazi kipya kilichopata mafunzo kinaendeleza mapambano, katika taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni.
Kifo cha kiongozi waBoko Haram Abubakari Shekau mwaka jana, katika mapigano na kundi la ISWAP kiliwatia moyo wanajeshi wa serikali, wengi walitumai kifo chake kingeashiria mabadiliko katika mzozo huo ambao umesabisha vifo vya watu takriban 40,000 tangu mwaka 2009 huku wengine zaidi ya milioni 2.2 kuwa wakimbizi wa ndani.
Katika miezi iliyofuata kifo cha Shekau, mamia ya wapiganaji walijisalimisha na viongozi wa eneo hilo walianza kufunga kambi za wakimbizi wa ndani, na kuwataka watu kurejea kwenye kaya zao.
Soma pia:Boko Haram yatwaa udhibiti wa jamii za katikati ya kaskazini mwa Nigeria
Baada ya muda huo ISWAP ilijipanga upya, na baada ya utulivu mfupi mashambulizi sasa yameanza tena kushuhudiwa.Licha ya kundi la dola la kiislamu kupoteza ushawishi nchini Syria na Iraq, Nigeria kwa sasa lipo mstari wa mbele.
Wachambuzi:Wanajihadi waimarisha udhibiti maeneo ya kimkakati
Mtafiti wa taasisi ya utafiti ya CNRS ya Ufaransa nchini Nigeria Vincent Foucher amesema, tawi la kundi la dola la kiislam Afrika magharibi ISWAP, linaimarisha udhibiti kwa maeneo muhimu vijijini, wakati jeshi la anga wakijiimarisha katika kuzima mashambulizi mijini.
Mtafiti huyo ameongeza kuwa kwa sasa kundi hilo linazidi kujitanua tangu lilipochukua maeneo yaliokuwa chini ya ushawishi wa Shekau.
Kwa upande wake mtafiti huru kuhusu mashambulizi ya kundi la dola la kiislam IS kote duniani amesema mashambulizi ya kundi hilo kwa sasa si kama hapo awali lakini wakati huo huo linafanya oparesheni endelevu ya kutwaa maeneo.
Mwezi Desemba wakati Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari akifanya ziara yake mjini Maiduguri wanamgambo hao wa jihadi walitekeleza shambulio la bomu la kurushwa ambapo idadi ya watu kadhaa walijeruhiwa.
Soma Pia:Wabeba silaha waua 3, wawateka 20 chuoni Nigeria
Muuzaji wa maji Abdulahi Isa 30, baba wa watoto watatu ambae yupo hospitalini akipokea matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya mikono yote katika shambulio hilo, anasema alichoshuhudia ni Roketi ilioanguka mbele yake.
Katika wodi ya wanawake jirani, Zahra Bulama, 40, alikuwa akijaribu kumfariji binti yake, Fatima mtoto wa miaka 10, kichwa chake kikiwa kimefunikwa na bandeji, analia na kulalama maumivu makali, alijeruhiwa katika shambulio lililofanywa na wanajihadi hao karibu na mji wao wa Konduga, ambapo watoto wawili kati ya wanane wa Zahra walikufa huku Fatma akipoteza jicho na sehemu ya uso wake.
Mtaalamu wa mazoezi tiba Sanda Mohammed, katika hospitali hiyo alisema bado wanapokea watoto walio na majeraha yasioweza kurekebishwa ambao maisha yao yamebadilishwa milele.
ISWAP Yawalenga wanaowaita vibaraka
Kundi hilo la itikdi kali linasema kuwa hailengi Waislamu moja kwa moja isipokuwa wawe washirika wa serikali au mashirika ya usalama. Lakini wachambuzi wanaonya kuwa kundi hilo linawangang'anya mamia kwa maelfu ya raia wa kawaida fedha.
kwa upande wake Gavana wa Borno Babagana Zulum alionya kuwa kundi hilo limejiimarisha kisasa zaidi na linafadhiliwa vyema, kuliko wapinzani wake.Ameongeza kuwa Jeshi la Nigeria linapaswa kujipanga upya ili kulishinda kundi hilo, vinginevyo wanamgambo hao wataendelea kuwa tishio kwa taifa zima.
Soma Pia:Maelfu wakimbia mashambulizi ya wabeba silaha Nigeria
Tangu mwisho wa Januari, jeshi limesema kuwa limewaua wapiganaji 180 na kuwakamata wengine 130 wanaoshukiwa kuhusika na ugaidi kaskazini mashariki.Mapema mwaka huu.
Wanajihadi hao walitoa video ya propaganda ya dakika 30, ikionesha kuwashirikisha wanajeshi watoto.
Hatua hiyo inatajwa na watafiti kuwa licha ya wapiganaji wakubwa wenye uzoefu kuuwawa, tayari kipo kizazi kipya ambacho kimeandaliwa kuendeleza mapambano ya jihadi.