1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kizazi kipya cha waalimu katika shule za Ujerumani

24 Mei 2012

Baada ya kusomesha kwa miaka ,waalimu wa shule za Ujerumani wanaotajikana kuwa wazee zaidi kuliko wenzao wa nchi jirani,wanatarajiwa kustaafu kwa wingi na kufungua njia ya kizazi kipya kuajiriwa.

Shule ya Sekondari yaAlbert-Schweitzer-Gymnasium mjini BerlinPicha: DW

Nchini Ujerumani,wakati huu tulio nao,yeyote aliyemaliza mafunzo yake ya ualimu anakuwa hana shida:matumaini ya kupata kazi ni mazuri.Baada ya kupita muda mrefu bila ya vijana kuajiriwa kufanya kazi hiyo,hivi sasa inaonyesha waalimu wengi zaidi wanahitajika kuliko hata idadi ya wale waliomaliza masomo yao katika vyuo vikuu.Na hasa katika fani ya sayansi na hesabu walimu vijana wana nafasi nzuri ya kuajiriwa.Sababu: waalimu waliozeeka wanastaafu kwa hivyo takriban wote wataondoka na nafasi zao zinabidi kuchukuliwa na waalimu vijana.Sura ya Ujerumani hii leo inaelekea katika shule moja ya mjini Essen katika jimbo hili la North Rhine Westfalia kumulika hali ikoje katika shule hiyo.

Niliamini moja kwa moja kwamba unapokuwa shuleni unaweza kuibadilisha dunia.Na hiyo ndio sababu iliyonifanya mie niamue kufanyakazi hii,wakati ule."Anasema mwalimu Thomas Helion anaesomesha mafunzo ya lugha ya kijerumani na sayansi jamii katika shule ya sekondari ya Frida Levy-Gesamtschule huko Essen.Yeye anajiangalia kuwa ni miongoni mwa waalimu wazee kati ya waalimu wenzake-kisiasa anajikuta katika kundi la wasomi wanaofuata mrengo wa shoto miongoni mwa walimu.Nywele na ndevu zake zimejaa mvi.Helion anakumbuka vyema zama zake,alipokuwa ndio kwanza anaaza kazi ,bado kijana , umri wake wakati ule ulikuwa kati kati ya miaka 20.Anakumbuka jinsi alivyosimama mbele darasani akijaa shauku na motisha.Kati kati ya miaka ya 70 ulikuwa wakati wa neema kwa waliosomea kazi ya ualimu. Wanafunzi wa hirimu tofauti waliandikishwa shuleni-na zaidi ya hayo mfumo wa elimu ukapanuliwa ili kuwaruhusu idadi kubwa zaidi ya watu kupata elimu ya juu.Shule mpya zikajengwa,idadi ya wanafunzi darasani ikapunguzwa ili waweze kuelewa vyema kile wanachosomeshwa:kwa ufupi watu wengi wakaajiriwa.Miaka michache baadae,mwishoni mwa miaka ya 70 mkakati wote huo ukasita,anasema mtafiti wa masuala yanayohusiana na shule na ambae pia ni mtaalam wa masuala ya elimu huko Essen,Prof Klaus Klemm anasema:

"Kulikuwa na wakati,naweza kusema hadi kati kati,kama si mwisnoni mwa miaka ya 80,ambapo wanafunzi,baada ya kupata shahada za chuo kikuu ,walikuwa wanaondoka na vilio kwasababu hawakupata maksi nzuri sana-wamepata nzuri tu na sio nzuri sana.Kwa namna hiyo wakitambua tangu mwanzo ",si hitaji kuanza chochote mie nikizingatia masomo nnayotaka kusomesha na maksi nilizopata."

Kilichotokea ni nini?Jibu ni kwamba,kile kijulikanacho kama " Vuguvugu la wenye kumeza vidonge" lilifika shuleni: Baada ya kuvuma ule mtindo wa uliokuwa ukijulikana kama "Baby-Boom" au "neema ya watoto" Ujerumani ikapatwa na pigo la kupungua idadi ya kizazi kipya.Kufumba na kufumbua idadi ya waalimu ikawa kubwa zaidi kuliko ile ya wanafunzi.Nafasi za kazi za ualimu zikawa adimu-hata wale waliomaliza masomo yao ya ualimu katika vyuo vikuu kwa shahada "nzuri sana" hawakuweza kuajiriwa.Hali hiyo ilikuwa ya aina yake nchini Ujerumani anasema Prof.Klaus Klemm anaendelea kusema:

"Walimu wa kijerumani,kwa sasa ndio wanaoangaliwa kuwa wazee,wakilinganishwa na walimu wengine katika medani ya dunia.Hali hiyo imesababishwa na kupungua kizazi kipya kupita kiasi ikilinganishwa na nchi jirani na Ujerumani.Nchini Japan kuna tatizo kama hili pia,lakini katika nchi jirani na Ujerumani hakuna hata katika nchi moja ambako hali ni mbaya kama huku."

Waalimu wa hirimu ya Thomas Helion walikuwa miaka nenda miaka rudi wakijikuta wao kwa wao tu.Walimu vijana hawakuwa wakiajiriwa sana.Sasa lakini Thomas Helion na waalimu wa hirimu yake wanastaafu.Yeye binafsi ana kama mwaka mmoja hivi kabla ya kumaliza.Katika daraja ya taifa,kila mwalimu mmoja kati ya wawili atastaafu katika kipindi cha miaka 10 hadi 15 ijayo:kwa maneno mengine,inamaanisha waalimu laki nne hao.Sasa waalimu watabidi waajiriwe.Kishindo lakini ni kwamba nafasi za kazi ya ualimu zimepindukia idadi ya waliomaliza masomo yao ya ualimu kataika vyuo vikuu.Wanafaunzi ambao kwa miaka wamekuwa wakisomeshwa na waalimu ambao wangeweza pengine kuwa mababu zao,watajikuta wakisomeshwa hivi sasa na waalimu ambao pengine umri wao ni mkubwa kidogo tu kuliko wao.

Mwanafunzi anyosha kidole darasaniPicha: picture alliance/APA/picturedesk.com

Hata katika shule ya sekondari ya Frida-Levy-Gesamtschule,waalimu wengi vijana wamekuwa wakiajiriwe mnamo miaka ya hivi karibuni.Wanafunzi wanafurahishwa na hali hiyo.Mwanafunzi mmoja wa kike anahisi waalimu wenye umri mkubwa baadhi ya wakati wanakuwa hawana motisha.

"Wamekuwa wakisomesha kwa muda mrefu hapa tena katika madarasa tofauti.Kama watoto wanafanya utundu baadhi ya wakati,basi mwalimu nae hakosi kushikwa na ugonjwa wa kichwa,kwa hivyo anakuwa mkali.Walimu vijana lakini ni wepya katika shule hii.Walimu watu wazima ni wapole pia,lakini vijana,sijui nisemeje,kuna kitu kinachowafanya waangaliwe kama wapole zaidi."Anasema mwanafunzi huyo wa kike.

Wengi wa waalimu hao vijana wanawajibika kupita kiasi.Zaidi ya hayo walimu hao vijana wanatumia teknolojia mpya na mtandao wa internet sawa na wanafunzi wao na wanaijua vilivyo mikondo inayojitokeza.

Waalimu wote wanabidi kushirikiana hivi sasa.Kunakosekana kizazi kati ya waalimu wenye umri uliopindukia miaka 50 na wale wenye umri wa chini ya miaka 35.Uzoefu,ushauri na hila waalimu watu wazima wanazoweza kuwapatia wenzao vijana ni changamoto kubwa kwa shule.Zaidi ya hayo masharti ya mtu kuweza kuwa mwalimu yamebadilika:Ikiwa katika enzi za Klaus Klemm shuleni takriban asili mia 7 ya walimu ndio waliosomea katika shule za sekondari za Gymnasium,hivi sasa idadi hiyo imeongezeka na kufikia asili mia 40.Walimu kwa hivyo wanajikuta wakisomesha madarasa yenye wanafunzi ambao uwezo wao ni tofauti na wanaotokana pia na tabaka tofauti za kijamii .KIzazi kipya cha waalimu hakijaaandaliwa vya kutosha kukabiliana na hali kama hiyo,anasema mwalimu mmoja kijana,Jan Buddeberg.Na ndio maana anasema anashukuru kupata ushauri kutoka kwa waalimu wenzao wenye maarifa.

"Kile ambacho tunaweza kujifunza ni jinsi ya kukabiliana na wanafunzi.Vipi nnaweza kukabiliana na wanafunzi wenye matatizo.Nifanye nini linapozuka sduala la nidhamu darasani,nifanye nini nnapokuwa na wanafunzi ambao hawasikii wanachoambiwa,wanafanya wanachotaka wao tu-nifanye nini mpaka na wao pia wavutiwe na masomo.Upande huo waalimu watu wazima wana maarifa na ustaadi ambao bado sisi hatunao."

Mwanafunzi wa chuo kikuu asomeya ualimuPicha: Fotolia/lightpoet

Jan Buddeberg ndio kwanza amekamilisha mtihani wake wa shahada ya pili ya chuo kikuu na anatafuta kazi ya ualimu-anataka kusomesha hesabu na falsafa.Watu wa hirimu yake ndio watakaojaza pengo litakaloachwa walimu watu wazima watakapostaafu-hadi pengine miaka 20 ijayo,pale zoezi hilo la kuwaajiri waalimu litakaposita.

Mwandishi: Hülsewig,Sola / Hamidou Oummilkheir

Mhariri: Moahammed Abdul-Rahman