1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kizungumkuti cha tamasha la Olimpiki kutokana na corona

11 Januari 2021

Asilimia 80 ya watu nchini Japan walioulizwa katika uchunguzi wa mashirika mawili katika siku chache zilizopita wanasema Olimpiki ya Tokyo inapaswa kufutwa au kuarihishwa, au wanasema wanaamini michezo hiyo haitafanyika

Japan Tokio Olympische Spiele verschoben  "Tokyo 2021"
Picha: Reuters/D. Ruvic

Asilimia 80 ya watu nchini Japan walioulizwa katika uchunguzi wa mashirika mawili katika siku chache zilizopita wanasema Olimpiki ya Tokyo inapaswa kufutwa au kuarihishwa, au wanasema wanaamini michezo hiyo haitafanyika. Uchunguzi huo ulifanywa na shirika la habari la Japaan Kyodo na Shirika la Utangazaji la Tokyo – TBS.

Matokeo hayo ni habari mbaya kwa waandalizi wa mashindano hayo na Kamati ya Kimtaifa ya Olimpiki – IOC wakati wakiendelea kusema tamasha hilo litafunguliwa Julai 23.

Tokyo inapambana na ongezeko la visa vya COVID-19 ambalo liliilazimu serikali kuu wiki iliyopita kutangaza hali ya dharura. Wakati akitangaza hali hiyo, Waziri Mkuu Yoshihide Suga alisema ana matumaini michezo ya Olimpiki itaendelea "Nadhani tamasha la Olimpiki linawezekana, kwa sababu utoaji wa chanjo umeanza kote duniani. Nataka kuanza kutoa chanjo hapa Japan mwishoni mwa mwezi ujao. Kama tutachukua hatua mwafaka, nadhani hisia za umma kuhusu olimpiki zitabadilika."

Mwishoni mwa wiki, Dick Pound ambaye ni mwanachama wa muda mrefu sana wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki alisema hana uhakika kama michezo hiyo itaendelea au la. "Nadhani hauwezi kuwa na uhakika kwa sababu suala kubwa kwa sasa ni ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona, lakini mpaka sasa hatua zote zinazohitajika ili kuandaa mashindano hayo zimechukuliwa. Maandalizi yote yanafanywa na kamati yenye uwezo mkubwa kabisa"

afp/reuters/ap/dpa