Klabu ya Arsenal yafuzu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
6 Mei 2026
Matangazo
Bao hilo la pekee lilifungwa na nahodha Bukayo Saka muda mfupi kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Hii ni mara ya kwanza katika muda wa miaka 20 kwa Arsenalkufika fainali ya michuano hiyo, mara ya mwisho ikiwa mwaka 2006 ambapo ilipoteza dhidi ya Barcelona.
Vijana wa Mikel Arteta sasa wanasubiri mshindi kati ya Bayern Munich na Paris Saint-Germain katika fainali itakayochezwa mjini Budapest Mei 30.
Ushindi huo pia unaiweka Arsenal katika nafasi nzuri ya kushinda mataji mawili msimu huu: Ligi Kuu ya Uingereza na Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.