Klabu za soka DR Kongo zatamba kimataifa
29 Septemba 2025
Klabu tatu za Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo zimefanya vizuri mwishoni mwa wiki kwa kupata ushindi kwenye mechi zao za mwanzo huku mabingwa wa DRC Les Aigles du Congo wakiondolewa kwenye mashindano ya mabingwa Afrika.
Klabu hizo zinazoshiriki mashindano ya mabingwa na shirikisho barani Afrika zilishuka dimbani Jumamosi na Jumapili, huku timu tatu zikifanya vyema kwenye raundi ya kwanza. Lupopo wakishiriki kwenye mashindano ya mabingwa Afrika, wamechomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Merreikh ya Sudan siku ya Jumamosi.
Klabu hiyo inaamini kufanya vyema kwenye mechi ijayo huko Libya ambapo watacheza mkondo wa marudiano kama alivyo ihakikishia DW msemaji wa Lupopo Daniel Ndongo.
"Tumefurahi sana kuifunga Al Merreikh nyumbani baada ya mechi ngumu . Al Merreikh ni Moja ya vilabu vyenye historia Katika bara la Afrika na tunajiandaa kwa mechi ya marudiliano kwa kujiamini, na lengo letu ni kushinda hulo. Klabu yetu inataka kufika hatua ya makundi ya mashindano hayo, na ili kufika huko tunahitaji kuzishinda timu Bora kama vile El Merreikh"
Les Aigles du Congo mabingwa wa kongo na wawakilishi wengine kwenye mashindano hayo kwa mara ya kwanza, wamekwaa kisiki huko Nigeria na kuzima ndoto zao za kufika hatua ya makundi baada ya kupoteza kwa goli 1-0 dhidi ya wenyeji wao Rivers united.
AS Simba ya Kolwezi wakishiriki kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya shirikisho, walipata alama 3 kwa kuwafunga 1-0 klabu ya Djabal, Maniema Union upande wao waliifunga klabu ya pamplemousses kutoka visiwa vya Morishazi Jumla ya mabao 2-1.
Wakiwa na matumaini ya kusonga mbele, klabu hiyo imedai kupeperusha vyema bendera ya nchi na kutakia heri kwa vilabu vya Kongo vinavyo wakilisha taifa. Blaise mwimba ni katibu wa maniema Union.
"Hiyo ndiyo furaha yetu sisi wote, hata tukienda kwenye visiwa vya morishazi tuweze kurudia na ushindi wa kutusaidia tupite kwenye hatua nyingine"
Tunapendelea pia kuwapa pongezi timu zingine rafiki kama vile lupopo ambao waliweza kuibuka na ushindi pia kwa goli Moja hata simba"
Mara kadhaa vilabu vya Kongo vinaondolewa kwenye mashindano ya kimataifa kabla ya robo fainali.
Ramdhani Kahambwe ni mchambuzi wa Michezo ambaye anaonesha wasiwasi wake kwa kilabu ya Lupopo na kuwapa nafasi Maniema Union.
Ramadhani. Mimi asilimia kubwa naipa klabu ya maniema Union kufanya vizuri ijapokuwa na kuondokewa na wachezaji wengi sana ambao ni wazuri na tegemezi kwenye klabu hiyo. Lupopo sema wana njia ngumu mbele Yao kwasababu ikitokea wakishinda kwenye Michezo yote miwili, ikitokea Orlando pirates na wenyewe wakafuzu basi Lupopo wanaweza kukutana na Orlando na wote tunajuwa ubora wa Orlando kuanzia ligi kuu ya Afrika Kusini mpaka kimataifa.
Vilabu vya Kongo vitacheza mechi zijazo ugenini.