1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoUreno

Kocha Martinez achukua majukumu ya Ureno

9 Januari 2023

Shirikisho la Kandanda la Ureno limemtambulisha Mhispania Roberto Martinez kuwa kocha mpya wa timu ya taifa. Martinez alijiuzulu kama kocha wa Ubelgiji baada ya kuondolewa katika Kombe la Dunia la Qatar

FIFA Fußball-WM 2018 in Russland |  Halbfinale -Frankreich vs Belgien
Picha: Reuters/H. Romero

Baada ya kombe la Dunia la Qatar, kuna makocha walioachishwa kazi, au waliojiuzulu, au waliostaafu, na kuzilazimu timu walizoziacha zikiwa katika hali ya kuanza upya. Miongoni mwa timu hizo ni Ureno ambayo leo imemteuwa Roberto Martinez kuwa kocha mpya, baada ya kujiuzulu kama kocha wa Ubelgiji baada ya kuondolwa katika Kombe la Dunia hatua ya makundi.

Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 49 anachukua usukani kutoka kwa Fernando Santos na suala la kipau mbele ambalo lazima kulishughulikia atakapoingia mlangoni ni kuiweka wazi hali ya nahodha Cristiano Ronaldo ambaye amesaini na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia.

afp

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW