Kocha wa Ghana alalamikia Penalti ya Ronaldo
25 Novemba 2022Kocha wa Ghana Atto Oddo amemkosa kocha Mmarekani ambae ametoa adhabu ya penalti ambayo imempa nafasi mchezaji Cristiano Ronaldo kuweka rekodi ya magoli katika mchuano wa Kombe la Dunia kwa kuiita hatua hiyo kama zawadi maalumu.
Ushindi wa Ronaldo katika nusu ya pili ya mechi kati ya Ureno na Ghana, unamfanya awe mchezaji pekee wa kwanza wa kiume kuibuka na ushindi katika michuano mitano tofauti ya Kombe la Dunia. Katika mechi hiyo Ureno ilipiga hatua kwa kuifunga Ghana mabao matatu kwa mawili.
Kocha Addo aelezea goli la "zawadi"
Kocha Addo amesikika akisema " kama mtu amefunga goli anastahili pongezi. Lakini goli hili kwa kweli ilikuwa zawadi maalum. Sina zaidi la kusema, ilikuwa ni zawadi maalum kutoka kwa kocha."
Ukosoaji huo wa moja kwa moja wa Addo kwa refa Ismail Elfath unaweza kumwingiza matatizoni na Shirikisho la Kandanda ulimwenguni FIFA. Na alipoulizwa sababu ya ushindi mwembamba na Ghana katika mechi hiyo pasipo kumun'gunya maneno alimtaja refa.
Addo anaamini kwamba mlinzi wa Ghana, Mohammed Salisu hakumchezea rafu Ronaldo, ambayo ingezusha mkwaju wa penalti.Na kulalamika kuwa maafisa hawakutumia chombo maalum cha kupitisha uamuzi uwanjani VAR kwa kuhakiki kitendo hicho.
Uchambuzi kuhusu timu za Afrika
Lakini mchambuzi wa soka ambae pia mtangazaji wa zamani wa DW, Sekione Kitojo anasema kama zilivyo timu nyingine za Afrika kwa hatua hii ya awali, Ghana imetumbukia katika mkondo wa wachezaji wake kutokuwa na maamuzi ya haraka wakati wakiwa uwanjani.
Baada ya goli la penalti, mshambulaji wa Ghana Andre Ayew aliwainua mashabiki wa timu yake baada ya kusawazisha bao hilo. Lakini katika kipindi kifupi baadae Urenu ilifanikiwa kuongoza kwa mabao matatu kwa moja, baada ya mabao ya Joao Felix na Rafael Leao. Lakini Osman Bukari alitaka kufufua matumani ya Ghana kwa kuifungia timu yake bao la pili katika dakika za lala salama.
Soma zaidi:Michuano ya Kombe la Dunia 2022 yazinduliwa rasmi
Ureno hivi kwa sasa ni kinara wa kundi H, mbele ya Korea Kusini na Uruguay, waliotoka sare ya bila ya kufungan katika mechi ya mwanzo. Mechi nyingine ya kundi H, Uruguay imelazimishwa kutoka sare ya bila ya kufungana na Korea Kusini lakini kwa kundi G, Brazil imeichapa Serbia mbili kwa moja.
Leo katika kundi B, Wales wataiita uwanjani Iran, Kundi A, Qatar watakutana na Senegal na kadahilia katika kundi hilo pia Uholanzi itafuana na Equador.
Vyanzo: AP/AFP