1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha wa Gladbach Rose kujiunga na Dortmund

15 Februari 2021

Kocha anayesifika sana wa  Borussia Moenchengladbach Marco Rose atachukua usukani wa wapinzani wao wa Bundesliga Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu. Klabu ya Gladbach imetangaza leo.

Deutschland | Bundesliga | VfL Wolfsburg v Borussia Mönchengladbach
Picha: Revierfoto/dpa/picture alliance

Kocha anayesifika sana wa  Borussia Moenchengladbach Marco Rose atachukua usukani wa wapinzani wao wa Bundesliga Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu. Klabu ya Gladbach imetangaza leo.

"Tumekuwa na mazungumzo mengi kuhusu mustakabali wa Marco katika wiki zilizopita. Inahuzunisha kuwa ameamua.-..kuwa angeüenda kujiunga na Dortmund katika msimu ujao wa joto,” amesema mkurugenzi wa spoti Max Eberl katika taarifa.

"Hadi wakati huo, tutaipa timu kila kitu ili kufikia malengo yetu msimu huu pamoja na Marco,” ameongeza.

Rose, mzaliwa wa Leipzig mwenye umri wa miaka 44, kwa muda mrefu alikuwa mstari wa mbele kumrithi kocha wa muda Edin Terzic katika benchi la Dortmund.

Baada ya kujiunga na Gladbach 2019, aliiongoza klabu hiyo ya Bundesliga kumaliza katika nne bora katika mwaka wake wa kwanza kabla ya kuwafikisha katika hatua ya mchujo ya Champions League kwa mara ya kwanza katika historia yao msimu huu.

Awalu alikuwa katika klabu ya Austria ya Red Bull Salzburg kwa miaka miwili, ambako alishinda mataji mawili ya ligi mfululizo.

Ijapokuwa Dortmund haijathibitisha uteuzi wa Rose, sasa anatarajiwa kutangazwa kama mrithi wa muda mrefu wa Lucien Favre, ambaye alitimuliwa Desemba.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW