1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Kandanda

Kocha wa Morocco aonya dhidi ya kuidharau Taifa Stars

5 Januari 2026

Kocha wa timu mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON 2025 Morocco Walid Regragui amewaonya wachezaji wake dhidi ya kuwapuuza wapinzani wao wasio na uzoefu Tanzania katika mchuano wao wa leo wa hatua ya mchujo.

Afrika-Cup 2025 | Alphonce Msanga wa Taifa Stars wakati wa mechi ya Uganda vs. Tanzania
Alphonce Msanga wa Taifa Stars wakati wa mechi ya Uganda vs. Tanzania Picha: Sebastian Frej/SFSI/IMAGO

Kocha wa timu mwenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON 2025 Morocco Walid Regragui amewaonya wachezaji wake dhidi ya kuwapuuza wapinzani wao wasio na uzoefu Tanzania katika mchuano wao wa leo wa hatua ya mchujo. Regragui amesema ukosefu wa unyenyekevu umewahi kuwagharimu katika mechi za huko nyuma.

Morocco ndio timu inayorodheshwa ya juu katika AFCON na wanapigiwa upatu katika michuano hiyo lakini kocha amesema vijana wake wanapaswa kuwa makini na kutoanguka tena kwenye mtego huo. Tanzania wanashiriki AFCON kwa mara yao ya nne na ni mara yao ya kwanza kucheza hatua ya mchujo.

Katika mechi nyingine ya leo, kocha wa Afrika Kusini Hugo Broos ameahidi "kutowaonea huruma" Cameroon atakapokutana na timu yake hiyo ya zamani. Broos aliiongoza Cameroon kutwa ubingwa wa AFCON 2017 nchini Gabon. Na sasa anasema kumbukumbu hizo zitabaki milele lakini mchuano wa leo utakuwa maalum kwake kwa sababu anataka kuipa ushindi timu yake ya Bafana Bafana.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW