1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kocha wa Ujerumani Loew apunguza wachezaji watano kikosini

Sekione Kitojo
8 Oktoba 2020

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew, amewapunguza wachezaji watano  kutoka katika  kikosi  chake ambacho kitakabiliana  na  Ukraine  na  Uswisi  katika  Ligi  ya Mataifa  ya  Ulaya.

Fußball | Nations League | Deutschland - Spanien
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim LoewPicha: picture-alliance/dpa/C. Charisius

Kocha  Loew  anaweka  mategemeo  yake  katika uzoefu wa  wachezaji wa Bayern Munich  na  RB Leizig  wanaorejea  katika  kikosi  hicho.

Ujerumani  imepoteza  uongozi mara tatu  katika  mchezo  wa  Uturuki na  kutosheka  na  sare  ya  mabao 3-3  siku  ya  Jumatano, ambapo Loew alichezesha  kikosi  cha  kujaziajazia kutokana na  wachezaji wake  wengi  kupewa  mapumziko.

Wachezaji wa timu ya Ujerumani iliyocheza na Uturuki wakishangilia baoPicha: Uwe Kraft/Imago Images

Ilikuwa  ni  mchezo  wa  tatu  mfululizo ambapo  Wajerumani walipoteza  uongozi  na  kumalizikia  kwa  sare. Pia  ilikuwa  ni mchezo  ambao  uliangaliwa  na  idadi  ya  chini  kabisa  ya  watu katika  TV  katika  tangu Loew  aanze akiifunza  timu  hiyo  ya  taifa miaka  14 iliyopita.

Benjamin  Henrichs, Nico Schulz, Niklas Stark, Nadiem Amiri  na mahmoud Dahoud, ambao  wote  walicheza dhidi  ya  Uturuki, wameondolewa  katika  kikosi  hicho kabla  ya  mchezo  wa Jumamosi  nchini  Ukraine na  mchezo  wa  nyumbani  dhidi  ya Uswisi  siku  tatu  baadaye.

Wachezaji wa  Bayern 

Loew atakuwa  na  wachezaji  wa  Bayern  Joshua kimmich, Serge Gnabry, Niklas Suele, Leon Goretzka na  mlinda  mlango manuel Neuer katika  kikosi  hicho cha  wachezaji 23 baada  ya kupumzishwa  pamoja  na  Marcel halstenberg  na  Lukas Klostermann  wa  RB Leipzig.

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ujerumani Manuel Neuer anarejea kikosiniPicha: Getty Images/A. Hassenstein

Mshambuliaji Timo Werner , ambaye  amepata nafuu  kutokana  na ugonjwa , pia  atarejea  kama ilivyo  kwa  mchezaji  wa  kati  wa Real Madrid Toni Kroos.

"Itakuwa  ni  muhimu  kushinda michezo  ijayo,"  Loew  alisema. "Kutakuwa  bila  shaka  na  timu tafauti kabisa uwanjani, kuliko  dhidi ya  Uturuki. Kila  mmoja  ana hamasa  na  morali  ya  kushinda."