Kofi Annan apendekeza tume huru kuchunguza matokeo ya uchaguzi
12 Februari 2008Matangazo
Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan ametaka kuundwe tume huru itakayochunguza matokeo ya uchaguzi wa tarehe 27 mwezi Disemba mwaka jana nchini Kenya. Kiongozi huyo amesema tume hiyo haitakiwi kuficha ukweli utakaojitokeza. Akizungumza katika bunge la Kenya hii leo Kofi Annan amewataka viongozi wa pande zinazohasimiana watafute suluhisho la haraka kwa mzozo wa kisiasa na kurejesha uthabiti nchini humo. Pia amependekeza kuwa suluhisho la kisiasa huenda lijumulishe kuundwa kwa serikali ya mseto.