1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kofi Annan atoa wito wa kuikoa Irak

19 Septemba 2006

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan, ameonya kwa mara nyingine tena kwamba kuna hatari kubwa Iraq kukumbwa kabisa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Akiuhotubia mkutano wa mawaziri wa mambo ya kigeni kabla ya mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa mataifa, Annan ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa ifanye juhudi kubwa kuisaidia serikali ya Iraq kutoka katika lindi la mchafuko .

Wito wa Kofi Annan kuisaidia Irak umekuja wakati polisi wakiendelea kugundua maiti za watu waliyouawa. Miili ya watu watatu imepatikana mashariki mwa mji mkuu Baghdad hii leo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW