Kolon. Siku ya vijana yaendelea nchini Ujerumani.
17 Agosti 2005Matangazo
Siku ya vijana wa Kikatoliki duniani inaendelea katika mji wa Kolon nchini Ujerumani, huku mamia kwa maelfu ya vijana kutoka duniani kote wakishiriki katika sherehe hizo za kanisa la Kikatoliki.
Jana maelfu ya vijana wa kikatoliki walisherehekea uzinduzi wa tukio hilo katika misa iliyofanyika katika uwanja wa mpira mjini Kolon.
Kiongozi wa kanisa hilo mzaliwa wa Ujerumani Pope Benedict wa 16 anatarajiwa kujiunga na sherehe hizo kesho Alhamis na kufunga tamasha hilo kwa misa kubwa ya wazi mjini Kolon hapo Jumapili.
Zaidi ya watu 400,000 wamejiandikisha kushiriki katika siku hiyo, na wahusika wanasema watu zaidi ya milioni moja huenda wakahudhuria katika wakati huu wa sherehe.