1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA AFRIKA LA KLBU BINGWA

11 Julai 2005

KOMBE LA KLABU BINGWA:

Maajabu yalizuka mwishoni mwa wiki katika kinyan’ganyro cha Kombe la klabu bingwa barani Afrika:Al Ahly ya Misri ndio timu pekee isioshindwa hadi sasa katika kinyan’ganyiro hiki.Al Ahly ilithubutu kuwazaba jana mabingwa wa Kombe hili Enyimba ya Nigeria tena nyumbani mwao mjini Eba kwa bao 1:0.Kwa ushindi huo,Ahly imeparamia kileleni mwa kundi A.

Mabingwa Enyimba wanaoania kutwaa kombe hili kwa mara ya tatu mfululizo na kuipiku TP Mazembe ya Kongo,ina pointi 1 tu hadi sasa wakati Ajax cape Town ya Afrika kusini ina pointi 2 baada ya kuizima Raja Casablanca na kutoka nayo suluhu bao 1:1 .

Katika Kundi B,mechi zote zilizochezwa hadi mwishoni mwa wiki, zilimalizika sare.Zamalek ya Misri nusra jana ikione kilichomtoa kanga manyoya. Nahodha wao Wael El Quabani lakini aliwaokoa wasishindwe nyumbani na Etoile du Sahel ya Tunesia.El Quabani alitia bao katika muda wa kufidia na kusawazisha .

Polisi walibidi kuingia uwanjani kumlinda rifu kutoka Afrika Kusini, Jerome Damon, kwavile wachezaji wa Etoile walikasirishwa na uamuzi wake wa kurefusha muda wa kufidia hadi dakika 6–hii iliwapa Zamalek nafasi ya kusawazisha.Duru ijayo ya Kombe la klabu bingwa, itachezwa Juali 22-24.

Mashindano ya ubingwa wa riadha ulimwenguni yatafanyika mwezi ujao wa August,mjini Helsinki,Finland.Kufuatia kutamba mwishoni mwa wiki kwa Paul Kipsiele Koech katika changamoto ya mbio za Golden League, mjini Roma ,chama cha riadha cha Kenya, kimeamua kumpa nafasi Koech kuiwakilisha katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi mjini Helsinki ili kuirudisha Kenya, ile medali ya dhahabu iliokwenda Gatar wakati wa mashindano yaliopita.

Chipukizi huyu mwenye umri wa miaka 23,alishindwa kufuzu kujiunga na timu ya wanakenya kwavile alimaliza wa 4 katika mashindano ya kitaifa hapo juni.

Kenya iliwachagua wanariadha 2 tu mwezi uliopita katika mashindano ya kitaifa. Koech,mshindi wa medali ya shaba wa olimpik, atajaza nafasi ya tatu ili kutoa changamoto kwa bingwa wa dunia mzaliwa wa Kenya anaekimbia chini ya bendera ya Qatar,Saif Saeed Shaheen.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW