1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA AFRIKA LA MATAIFA:

26 Januari 2004

KENYA YALAZWA MABAO3:1 NA MALI NA SENEGAL BURKINA FASO UWANJANI BAADAE LEO KAMERUN NA ALGERIA ZATOKA SULUHU 1:1 GUINEA YAILAZA KONGO 2:1 NA MISRI YAITOA ZIMBABWE 2:1.

Hayo na pamoja na maoni ya mashabiki huko Afrika mashariki na kati juu ya Kombe la Afrika ndio niliowaandalia jioni hii:
Leo ni siku ya tatu ya Kombe la Afrika la mataifa nchini Tunisia:Harambee Stars-Kenya-muakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki wameingia uwan jani alaasiri ya leo kucheza na Mali,mwenyeji wa kombe lililopita la Afrika la mataifa.

Kenya imezabwa mabao 3:1 na Mali katika uwanja wa Bizerte.
Mali iliufumania kwanza mlango wa Kenya tayari mnamo dakika ya 28 ya mchezo pale Mohamed Sissoko aliponasa bao lwa kwanza la Mali.Harambee Stars wakajibisha baada ya mapumziko kwa bao la Robert mambo. Ufunguo wa ushindi wa Mali ni stadi wa Tottenham Hotspurs ya Uimngereza Frederic Kanoute alieipatia mali bao la pili na la 3 mnamo dakika ya 63 na ya 81 ya mchezo.tayari sakika ya 80 ya mchezo,Kenya ilikaribia kusawazisha.

Mpambano wapili jioni hii ni kati ya Burkina Faso na Senegal-timu iliotamba katika Kombe lililopita la dunia na maka mo-bingwa wa Afrika.
Senegal jioni hii ikiongozwa na mshambulizi wake hatari El hadji Diouf,inas azma moja tu-ushindi dhidi ya Burkina Faso na hivyo kuthibitisha kuwa enzi ya simba wa nyika Kamerun imeanza kumalizika na wao ndio simba hasa wa nyika barani Afrika.Diouf ametia fora katika dimba la Afrika tangu alipoiongoza senegal kumaliza nyuma ya kamerun au nafasi ya pili katika Kom be lililopita la Afrika nchini Mali.

Senegal inaongozwa na mfaransa mwengine Guy Stephan aliechukua uongozi wa timu kutoka kwa Bruno Metsu alieichukua Senegal hadi robo-finali ya kombe la dunia ilikopigwa kumbo kwa bao la kitanzi-golden Goal-na Uturuki.Kati ya mapambano ya ke 9 ya taifa, Stephan ameshinda 5 la mwisho dhidi ya bafana bafana au afrika kusini inayoteremka uwanjani kesho dhidi ya Benin. Stephan amekuwa kocha wa Lyon na Bordeaux na kama m chezaji alivaa jazi za Rennes,Le Havre,Orleans na Caen.Azma yake sasa ni kuitawaza Senegal mabingwa wa Afrika.Kwahivyo, changamoto ya jioni hii dhidi ya Burkina faso -wenyeji wa Kombe la Afrika 1998 ni ishara ya kwanza kwa Senegal katika kampeni yao.Burkina Faso lakini haitasalim amri kwa urahisi na imeahidi kuzima vishindo vyote vya wasenegali.

Jana simba wa nyika walizimwa kunguruma na Algeria.Licha ya kutamba na kudhibiti mchezo,Kamerun iliondoka suluhu na kugawana pointi na Algeria kwa kuchapana bao 1:1.Mnamo dakika ya 44 ya mchezo Patrick Mboma alibomoa lango la Algeria alipoutia kichwa mpira wavuni kutoka m kwaju maridadi alioupiga Geremi.

Tofauti kabisa na mkondo wa mchezo,Algeria ilisawazisha püale mlinzi wao Zafour alipouchapa mkwaju mkali katika lango la kamerun kufuatia kona ilioelekezwa katika lango hilo.Mashabiki 20,000 uwanjani wengi wao waalgeria waliovuka mpaka tu kushuhudi changamoto hiyo walishangiria.Hadi wakati huo nahodha wa Kamerun,Rigobert Song,alijenga ngome yake imara kabisa na kutowapa nafasi hata kidogo washambulizi wa Algeria.Baada ya bao hilo,Algeria ilipunguza kasi na kuanza kujilinda tu na walibahatika pale Atouba alipogonga mwamba wa lango lao kwa kichwa mnamo dakika ya 64 ya mchezo na tena pale Samuel Eto'o alipoupiga mpira kinyume-nyume karibu na lango la Algeria na kupita kidogo tu juu ya lango la Algeria.

Wakicheza na Eto'0 usoni, Geremi wa Chelsea na Eric Djemba -Djemba ,kati ya uwanja simba wa nyika walifanya kila kitu isipokua kunguruma kwa mabao.Kamerun lazima ishinde mpambano ujao na Zimbabwe ,kwani changamoto na Misri haitakua kuteremka mlima.
Misri imeparamia kundi hili C kufuatia mabao ya Tamer Abdelhamid na Mohammed Barakat.Lakini ilikua Peter Ndlovu alieufumania kwanza mlango wa Misri wanaoania taji lao la 5 la Afrika.

Guinea imejiunga na wenyeji Tunisia kileleni mwa kundi A kwa kuwazaba simba wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo mabao 2:1.kama Zimbabwe, kongo ilitangulia kutia bao,lakini Guinea iliwaambia wakongo 'kutangulia jamani sio kufika.'Katika dimba la ufunguzi hapo jumamosi, wenyeji Tunisia,walitokwa na jasho kabla kuwaangusha chipukizi Rwanda kwa mabao 2:1.
huko Tunisia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW