1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA AFRIKA MASHARIKI NA KATI KIGALI

28 Novemba 2005

Zanzibar imeistusha Ruanda,mwenyeji katika ufunguzi wa kombe la Challenge cup la afrika mashariki na kati mjini Kigali, jumamosi kwa kuizaba bao 1:0. Kenya haikuwasili firimbi ilipolia.

Ligi mashuhuri za Ulaya:

Katika Bundesliga-Bayern Munich imefungua mwanya wa hadi pointi 6 kileleni kufuatia ushindi wao wa mabao 2:1 jumamosi dhidi ya Mainz kwenye uwanja wa Allianz Arena.Huo ni ushindi wa 12 mfululizo katika mechi 14 ikiwa ni rekodi tangu kuanza msimu wa Ligi.Werder Bremen inayofuata nafasi ya pili ilikiona cha mtema kuni ilipzabwa mabao 2-1 na Schalke 04.

Hamburg ilipanda juu kwa pointi 2 kuifuatia Bremen kufuatia ushindi wao wa bao 1:0 dhidi ya bayer Leverkusen.Hamburg timu pekee iliothubutu kuilaza Bayern munich msimu huu iko pointi 6 nyuma ya mabingwa Munich.

Stuttgart inaendelea kupepesuka na ilimudu kwa mashaka sare bao 1:1 na Eintracht Frankfurt.Berlin jana ilitoka nyuma baada ya kuchapwa mabao 2 na mwishoe kusawazisha 2:2 na Borussia Mönchengladbach.

Katika Ligi ya Uingereza-Premier League,Wayne rooney alipeperusha kileleni Manchester united hadi nafasi ya pili nyuma ya Chelsea kwa kuipatia ushindi wa mabao 2:1 dhidi ya West Ham.

Katika La Liga-Ligi ya Spain,mkameroun Samuel Eto’o anaendelea kutamba alipofungua mlango wa ushindi wa FC Barcelona wa mabao 4-1 jana dhidi ya Racing Santander.Akiongoza orodha ya watiaji magoli kwa mabao yake 11, Samuel Eto’o alifuatwa na wenzake akina Ronaldinho,Lionel Messi na Silvinho.

Jumamosi ilikua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu alitia gongo-mkutano uwanjani mjini Kigali,Ruanda.Wenyeji Ruanda walifungua dimba la Kombe la Challenge cup kwa Afrika mashariki na kati linaloingiza timu 10 au 11 ikiwa Kenya mwishoe, ingewasili Kigali.Kenya imekumbwa na mzozo wa madai ya fedha kutokla wachezaji wake. Ruanda ilizabwa bao 1:0 na Zanzibar Heroes .Licha ya ushindi wa bao 1:0 dhidi ya Ruanda mjini Kigali,Zanzibar Heroes, wamekataliwa uwanachama wa CAF-shirikisho la dimba la Afrika, mpaka kwanza FIFA imeipa Zanzibar uanachama.Vilabu vya Zanzibar,vitaruhusiwa hatahivyo, kushiriki katika vikombe vya mabingwa wa Africa m simu ujao.

Ziara ya ujumbe wa ZFA na TFL mjini Cairo,kwahivyo, haikuzaa matunda mema.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW