KOMBE LA AFRIKA
9 Februari 2004Matangazo
Timu 4 zilizokata tiketi zao za nusu-finali ya kombe hili sasa zinajulikana:wenyeji tunisia walioitoa Senegal jumamosi kwa mabao 2:1 , Mali walioitum Guinea kwa bao 1:0,Nigeria waliowazima simba wa nyika-Kamerun kunguruma jana kwa mabao 2-1 na mwishoe,Morocco iliozima vishindo vya Algeria kwa mabao 3-1 katika mpambano wa kwanza kurefushwa wakati katika Kombe hili la 24 la Afrika. Kwahivyo, jumatano hii: Nigeria itacheza na Tunisia na Morocco na Mali.Finali itakua jumamosi ijayo katika uwanja wa Rades,mjini Tunis ambapo bila shaka atatawazwa bingwa mpya. Nigeria sasa ndio inayopigiwa upatu kurejea ushindi wao wa miaka 10 nyuma mjni Tunis walipoilaza Zambia katika finali-kwani wao ndio waliothubutu kuwazima simba wa nyika jana wasingurume licha ya kwamba ni simba waliotangulia kutia bao. Enzi ya miaka 4 ya simba wa nyika kileleni mwa dimba la Afrika ilimalizika jana .Kamerun ikitapia taji lao la 3 mfululizo na la 5 kwa jumla,lakini Nigeria ilibisha. Nigeria ambao haikuwahi kutolewa nje ya robo-finali katika vikombe 9 vilivyopita,ilibidi kutoka nyuma na kuondoka m wishoe na ushindi wa mabao 2:1.Muda mfupi kabla kipindi cha mapumziko,Nigeria ilisawazisha pale J.J.Okocha nahodha wao alipochapa mojawapo ya mikwaju yake maarufu ya free-kick hadi porini mwa simba wa nyika bila ubishi wowote wa kipa wao.Halafu John Utala akaupiga msumari wa mwisho katika jeneza la Kamerun mnamo dakika ya 73 ya mchezo.Ilikua samuel Eto'o na sio patrick Mboma aliebomoa kwanza lango la Nigeria,lakini wao walisema tulia:Jibu la Nigeria halikukawia -kwani kufuatia madhambi ya kipumvbavu ya mlinzi wa kamerun,J.J.Okocha alisawazisha.bao la pili la nigeria lilitokana na stadi wa arsenal london, Mwamko Kanu aliemtpia Utaka kumaliza udhia.Ushindi wa jana umeirudisha Nigeria kileleni licha ya pigo iliopata katika mpambano wake wa ufunguzi. Nahodha was kamerun Rigobert Song baada ya mechi ya jana amewaonya mahasimu wa simba wa nyika kutowatoa kabisa maanani kwa kuwa tu jana simba waliteleza na kunaswa wavuni.Song alisema sababu ya simba kutonguruma jana ni dhana mbovu ya hisia za kutoshindwa ilioanza kuingia vichwani mwa wachezaji wa timu yake,lakini sasa wamefunzwa darasa na Nigeria na hii itawasaidia kukata tiketi yao kwa Kombe lijalo la dunia hapa ujerumani 2006. Kocha wa Kamerun , mjerumani WINFRIED SCHÄFER alietia saini mkataba mpya kabla kuanza Kombe hili la Afrika,ameahidi kuwa simba wa nyika watarudi kunguruma.""icha ya pigo hilo waliopata Kamerun bado ni timu kali katika dimba la dunia""alidai Schäfer.Akasema hana dhamiri ya kujiuzulu.Alisema simba watafufuka. Katika changamoto ya pili ya kusisimua jana, Algeria walikua wamershafunga virago kwa safari ya nusu-finali,laskini dakika ya mwisho bao la Abdelmalik,mzaliwa Ufaransa la dakika ya 84 ya mchezo,lilizimwa na Chammakh aliejikuta pekee na kuusindikiza mpira wavuni.Kuanzia hapo,walikua wamorocco tu waliohanikiza uwanjani mpira uliporefushwa.Hadji na zairi wakwabadilisha mkondo mzima wa mchezo na kuwaarifu waalgeria waliowatoa Misri kwamba 'leo bahati si yenu'. Morocco inaingia sasa nusu-finali kwa mara ya kwanza tangu 1988 na wakitwaa Kombe itakua kwa mara ya pili tangu 1976 mjini Addis Ababa. Polisi wa Tunisia walikua na kazi pevu kupambana na mashabiki waliokasirika wa Algeria uwanjani Sfax.Machafuko yao yalianza mara tu hadji alipotia bao la pili la Morocco.Sehemu ya uwanja ambayo walisheheni mashabiki 20.000 wa Algeria,ilianza kuharibu viti vya kukalia mashabiki na kurusha uwanjani huku wakiona ndoto yao ya Algeria ikififia na kutoweka. Kinyume na Algeria, mjini Rabat na katika miji mingine ya Morocco,ilikua 'halua-halua'- -utamu-utamu na kushangiria mikahawani na majiani.Mashabiki walisema na huu ndio mwanzo tu-kuna mengi zaidi yanakuja. BUNDESLIGA: Mabingwa Bayern Munich jana walirudi kutamba tena walipoikomea Hannover 96 mabao 3-1 na kupunguza mwanya wao na viongozi wa Ligi Werder Bremen hadi pointi 6. Bremen waliondoka na ushindi mwengine mara hii wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Mönchengladbach.Ushindi wa Bremen na bayern munich ni muhimu sana kwavile wapinzani wao 2 wa karibu sana - Stuttgart na Bayer Leverkusen wote walipatwa na msukosuko.Stuttgart walikandikwa bao 1:0 na Berlin inayoburura mkia na Leverkusen ikazimwa na Frankfurt. Katika Ligi ya Uingereza,Manchester united ilikomea Everton mabao 3-0,lakini mwishoe, Everton ilirejesha mabao hayo na kuondoka suluhu na Manchester 3:3.. Nchini Spain, Real Madrid na valencia zote ziliondoka na ushindi na kuacha hali ile ile kileleni mwa Ligi.Ronaldo na Roberto carlos walitia mabao kila mmoja katika ushindi wa 2:1 wa Real dhidi ya Malaga.Valencia hawakutokwa na jasho kuizima Atletico madrid kwa mabao 3-0.
Matangazo
