KOMBE LA ASIA LA DIMBA LAANZA JUMAMOSI HII NCHINI CHINA: BRAZIL YAKOMEWA 2:1 PARAGUAY KATIKA COPA AMERIKA NA TANZANIA YAJITOA KATIKA UBINGWA WA RIADHA WA AFRIKA BRAZZAVILLE.
15 Julai 2004MICHEZO :
Kufuatia kombe la Afrika la Mataifa nchini Tunisia, mapema mwaka huu na baadae Kombe la Ulaya nchini Ureno mwezi uliopita,leo ni zamu ya Kombe la Asia la Mataifa linaloanza nchini China .China yataka kuiigiza Ugiriki kutoroka na Kombe.Zinazopigiwa upatu lakini kuwika ni mabingwa mara kadhaa Saudi Arabia, Iran na hata Japan.
Mashindano yataoneshwa hadi majumba zaidi ya milioni 500 kote barani Asia,Mashariki ya kati na kwa mara ya kwanza hata huku Ulaya.World Sport TV imetia saini mapatano na umoja wa TV wa nchi za kiarabu ASBU kuionesha dimba hilo uarabuni.timu zinazowakilisha kanda hiyo ni Saudi Arabia, Iran,Qatar,bahrein,Umoja wa Falme za kiarabu,Jordan,Iraq na Oman.
Jumla ya mechi 32 zitachezwa nchini China, ambayo inalitumia kombe hili la bara la Asia nchini mwake, kufungua pazia kwa michezo ya olimpik ya mwaka 2008 itakayofanyika China baada ya hii ya mwezi ujao nchini Ugiriki.Ugiriki ikiikaribisha michezo ya Olimpik kurudi nyumbani ambako ni asili yake, ilitoroka na Kombe la Ulaya la mataifa huko Ureno kwa msangao wa timu zote 16.China kwahivyo, yataka kufuata nyayo za wagiriki.Japan,saudia Arabia na Iramn kwahivyo, zafaa kuchunga,kwani dimba limewasili China.
Copa Amerika, Kombe la Amerika Kusini tayari limezusha msangao wake wa kwanza kati ya wiki hii:mabingwa wa dunia Brazil walizabwa juzi mabao 2-1 na Paraguay.P igo hilo limemaliza rekodi ya kocha Parreira wa Brazil ya kutoshindwa katika mashindano 15 mfululizo.Paraguay imeibuka juu ya kundi hili,huku Brazil ikifuata mnyuma nafasi ya pili.Paraguay itakumbana kesho katika robo-finali na Uruguay wakati Brazil wana ahadi na Mexico.
Tanzania kati ya wiki hii ilijitoa nje ya mashindano ya ubingwa wa riadha wa afrika huko Kongo-Brazzaville.sababu iliotoa tanzania ni shida za fedha.Mwenyekiti wa chama cha riadha cha tanzania (TAAA) Elius Sulus amenukuliwa kusema,
"Tumeamua kujitoa baada ya kushindwa kukusanya Shilingi za Tanzania milioni 5.5 hizo ni sawa na dala alfu 5 kugharimia usafiri."
Sulus akaongeza kusema kwamba, Tanzania sasa inajishughulisha kushiriki katika mashindano yajayo ya olimpik mjini Athens,Ugiriki,inayoanza August 13 hadi 29.
Hatahivyo, Elius Sulus, ameungama kwamba mashindano haya ya siku 5 mjini Brazzaville,yangeisadia Tanzania kujinoa kwa michezo ijayo ya Olimpik. hata katika michezo ya Olimpik, kikosi cha Tanzania kitakua kidogo. Tanzania imefifia kimichezo tangu katika dimba hata katika riadha.Philbert Bayi,bingwa wake mashuhuri katika medani ya riadha aliipatia Tanzania medali ya fedha ya Olimpik katika masafa ya mita 3000 kuruka viunzi baada ya kuongoza hadi mita 150 usoni na baadae kupokonywa ushindi Mpoland Malinowski.Kenya,iliisusia michezo ile.
Mbio za baiskeli za TOUR DE FRANCE zikiwasili nusu-njia ,yadhihirika kwamba Muamerika Lance Amstrong atanyakua ubingwa wake 6 mfululizo na hii ikiwa ni mara ya kwanza kushinda namna hivyo.Kwani baada ya hatua 10 kati ya zote 20,Amstrong ameshajenga nguvu zake wazi kuwapiku mahasimu wake wakubwa katika milima ya Pyrenees na Alps-miongoni mwao ni jan Ulrich wa Ujerumani.
Mpinzani mwengine aliopo nafasi ya pili wakati huu ni Muamerika Hamilton.Yeye alikuwa hadi kati ya wiki hii nyuma ya Amstrong kwa sek.43 wakati Ullrich yuko nyuma alikuwa seku.55.
Jan Ullrich amesema mbio hizi za Tour de France, zitaamuliwa sio kwa sekunde bali kwa dakika.Amstrong anafurahia kwamba jumamosi hii huenda akavaa jazi ya manjano pale mbio hizi zinapoingia leo katika hatua ya pili ya milima ya Pyrenea.