1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA CHALLENGE CUP ETHIOPIA LAENDELEA:UJERUMANI KUCHEZA KESHO NA THAILAND MJINI BANGKOK

Ramadhan Ali20 Desemba 2004

KOREA KUSINI YAIZABA UJERUMANI MABAO 3-1

NUSU FINALI YA CHALLENGE CUP MJINI ADDIS ABABA ITAKUA KATI YA ETHIOPIA NA KENYA NA SUDAN BURUNDI

SANTOS NI MABINGWA WAPYA WA BRAZIL

NAABEBE DINKESSA ASHINDA MBIO ZA NYIKA ZA SHIRIKISHO LA RIADHA ULIMWENGUNI (IAAF) BRUSSELS

Korea ya Kusini ilisangaza jana Ujerumani ilipoizaba mabao 3:1 na hivyo kulipiza kisasi chja nusu-finali ya kombe la dunia 2002.Ushindi huo umeitia moyo timu hiyo chipukizi ya wakorea Kusini inayoandaliwa kwa Kombe lijalo la dunia 2006.Hilo limekuwa pia pigo la kwanza kwa timu ya taifa ya ujerumani chini ya kocha wake mpya Jürgen Klinsmann aliechukua uongozi wa timu hii kutoka kwa

Rudi Völler kufuatia kupigwa kumbo na mapema Ujerumani nje ya Kombe la ulaya la mataifa hapo juni mwaka huu huko Ureno.

Korea ya kusini chini ya kocha Jo Bonfrerre kutoka Holland, iliufumania kwanza malngo wa ujerumani pale mchezaji wao wa kiungo Kim Dong-Jin alipouchapa mkwaju mkali ndani ya wavu wa lango la Ujerumani mnamo dakika ya 16 ya mchezo.Nahodha wa ujerumani Michael ballack akasasazisha dakika 8 baadae kwa

Lakini,mnamo dakika ya 70 ya mchezo,mshambulizi wa Korea kusini Lee Dong-Gook,alitia bao maridadi ajabu lililomuacha kipa Oliver Kahn akizubaa hajui afanye nini.Ujerumani ilikaribia kusawazisha kufanya 2:2 mnamo dakika ya 85 ya mchezo,lakini mkwaju wao wa penalty haukunasa wavuni mwa lango la Korea ya Kusini.haukupita muda,wakorea wakakamilisha ushindi wao wa mabao 3:1 la Ujerumani.Ujerumani iliizaba Japan,mabingwa wa Asia mabao 3:1 katika mechi yao ya kwanza.

Ujerumani inakamilisha keshi ziara yake hii ya bara la asia ikiwa na miadi mjini Bangkok na Thailand.

Thierry Henry,stadi wa Ufaransa anaeichezea Arsenal London,anatazamia kusikia leo iwapo atakua mchezaji wa kwanza anaecheza dimba Uingereza kuteuliwa ‘Mwanasoka wa mwaka wa FIFA’-shirikisho la dimba ulimwenguni.

Henry anashindana na Muukraine Andriy Shevchenko aliemshinda wiki iliopita kutwaa ‘taji la mchezaji bora wa mwaka wa dimba wa Ulaya’.Henry alikuja wapili nyuma ya Zinedine Zedane wa Real madrid katika taji la mwaka jana 2003.Msimu uliopita, Henry alitia jumla ya mabo 38 na thelethini kati ya hayo katika Ligi ya uingereza peke.

Mashindano yote ya dimba barani Ulaya,yanapangwa kukamilishwa hadi Mei 14,2006 ili kuwahifadhi wachezaji wasiumie au wasichoke kitakapoanza kinyan’ganyiro cha kombe la dunia hapa Ujerumani 2006.Hii iliamuliwa jana na halmashauri-tendaji ya FIFA mjini Zurich.

FIFA iliamua pia jana kwamba mchezaji dimba mashuhuri kabisa wakike wa Mexico,haruhusiwi kucheza katika dimba la malipo la timu za wanaume katika daraja ya pili ya Ligi ya mexico.FIFA imesisitiza kwamba,lkazima pawepo tofauti kati ya ligi za wachezaji wa kiume na wachezaji wakike katika dimba.

Klabu ya PELE-SANTOS ni mabingwa wapya wa Brazil na hii ni kwa mara ya pili kutoroka na ubingwa mnamo muda wa miaka 3:

Santos ilizaba jana Vasco da gama mabao 2-1 katika fimnali.Kocha wao Vanderlei Luxemburgo,kocha wa zamani wa Brazil, ambae msimu uliopita aliiongoza Cruzeiro kutawazwa mabingwa,alinyakua taji lake la 5 jana alipoitawaza SANTOS klabu ya zamani ya Pele mabingwa wa Brazil.

NUSU_FINALI YA KOMBE LA AFRIKA MASHARIKI NA KATI ADDIS ABABA:

Wenyeji Ethiopia waliizaba jana Zanzibar mabao 3:0 katika kipindi cha pili na sasa wameingia nusu-finali ya kombe hilo wakiwa na miadi na Kenya jumatano hii ijayo.

Waethiopia walikabiliwa na lazima ya kushinda m bele ya rwanda ilioizaba Tanzania-bara mabao 5-1 hapo kabla, ili waingia nusu-finali kutoka kundi B.

Ushindi huo sio tu umewahakikishia tikiti ya nusu-finali nyumbani Addis,bali pia umewaweka kileleni mwa kundi lao wakiwa na jumla ya pointi 10 wakifuatwa na Burundi.

Zanzibar imefanya bora zaidsi katika mashindano haya kuliko wenzao Tanzania-bara.zanzibar ilizima vishindo vya waethiopia jana katika kipindi cha kwanza hadi pale Fekru Tefferra alipozima ubishi wa wazanzibari mnamo dakika ya 61.Dakika 4 baadae,Grima,mchezaji wao wa mwaka 2003 aliponguruma langoni mwa zanzibar.Mwishoe Hider Mensur akawasindikiza nae wazanzibar nyumbani kwa bao la 3.

RIADHA:

:Abebe Dinkessa wa ethiopia, jana alishinda mbio za nyika za shirikisho la riadha ulimwenguni huko Brussels,Ubelgiji.Dinkessa alikamilisha masafa ya mita 10.5000 kwa muda wa dakika 33 na sek.22.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW