KOMBE LA DUNIA-GHANA !
26 Juni 2010Matangazo
Raundi ya pili ya mashindano ya kombe la dunia inaanza leo nchini Afrika Kusini ambapo timu16 zitashiriki .
Leo Ghana itapambana na Marekani na Uruguay itachuana na Korea ya Kusini.Ghana ndiyo timu pekee ya Afrika iliyobakia katika mashindano ya kombe la dunia.
Ikiwa itafanikiwa kuilaza timu ya Marekani Ghana itakuwa nchi ya tatu ya kiafrika kuingia katika robo fainali baada ya Cameroon na Senegal.Hapo jana bingwa wa Ulaya Uhispania ilifanikiwa kuingia katika raundi ya pili, baada ya kuibwaga Chile kwa mabao mawili kwa moja.
Licha ya kubwagwa, timu ya Chile pia itashiriki katika raundi ya pili.