1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la Dunia: Je, DRC itafanikiwa kufuzu?

Saumu Njama Zuberi Ally
13 Oktoba 2025

Mechi za kufuzu kombe la Dunia ziliendelea, DRC ilitoa kichapo huko Lomé huku matumaini yakufuzu yakisalia kwenye mizani.

Kandanda | DRC
Wakongomani wanaamini bado timu ya Taifa ina nafasi ya kushiriki kwa mara ya pili kwenye kombe la Dunia.Picha: Fadel SennaAFP/Getty Images

DRC ilishinda mechi dhidi ya Togo ijumaa Kwa bao 1-0 , nakurudisha  matumaini Kwa DRC  kufuzu kwenye kombe la Dunia baada ya kupoteza dhidi ya Senegal, mechi ambayo Kwa wakongomani ilikuwa mlango pekee wa kuingia kombe la dunia.

Kwa baadhi ya wakongomani wanaamini Kongo bado inayo nafasi ya kwenda Kwa mara ya pili kwenye kombe la Dunia.

Masudi David na Kayumba Eric ni mashabiki wa timu ya taifa,  "Ushindi unamanifaa Kwa ukubwa kwasababu tulikuwa tunauhitaji ili kujihakikishia kupata nafasi ya  kuweza kumpatia presha Senegal. Soka inakuwaga na maajabu yake, na lolote linaweza likatokea Senegal akatandikwa na sisi tukamtandika Sudan na tukachukuwa tiketi kibabe na tukaenda kushiriki mashindano" alisema David

"DRC kupita Moja Kwa Moja hilo tusaau kwasababu nafasi waliokuwa nayo ni dhidi ya senegali na hawakutumia nafasi hiyo vizuri na unajuwa kwenye soka Wakati mnapata fasi kama hiyo mnatakiwa kutumia vizuri kwasababu sioni timu ya Senegal kufungwa." Kayumba aliongezea.

Baada ya ushindi huo, kocha  Sebastian Desabre anaamini kuwa timu yake itaenda kwenye hatua ya mchujo, "Kwetu sisi tunafikiria kuwa tukishinda mechi tatu zinazo tutaenda kwenye mchujo wa kombe la Dunia"

DRC inajiandaa kukipiga dhidi ya Sudani kesho Wakati wakiombea Senegal ifungwe au Kongo ichukuwe nafasi ya timu 4 zitakazo pambana kutafuta timu itakayoenda kwenye mchujo .

Ramazani Kahambwe mchambuzi wa michezo anatoa maoni yake kuhusu timu ya Kongo,  "Matumaini yetu ni makubwa sana kufuzu kama mshindi Bora wa nafasi ya pili,   Kongo asilimia kubwa huwa tunapita tukiwa na kikokotoo mkononi, lakini ile ya kusema kwamba hii mechi tunauhakika nayo Kwa asilimia mia mara nyingi huwa atufuzu."

"Siyo kazi rahisi lakini ukiingia vitani lazima ujipange kwaajili ya mapambano. Hayo Mataifa mengine nao pia wanajuwa kwamba Afrika Kuna Watu watatoka huko ni wahatari sana. Hata hivyo, DRC bado safari ni ndefu kwani timu 4 zitachuana ili kutafuta timu Moja itakayo wakilisha Afrika kwenye mchujo utakao shirikisha mabara tofauti"

Bara la Afrika litawakilishwa na timu tisa zitakazo fuzu moja kwa moja, tano miongoni mwao tayari zimejikatia tiketi zao, nazo ni  Tunisia, Moroko, Algeria, Misri na Ghana.

Mnamo mwaka wa 1934, Misri ilikuwa timu ya kwanza ya Afrika kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia. Wakati DRC, ikijulikana kama   Zaire Ilishiriki  katika michuano hiyo mnamo mwaka 1974, na kuwa timu ya kwanza ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kufuzu.

Senegal inaongoza  Kundi B, na alama 21. huku DRC ikichukuwa nafasi ya pili na alama 19.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW