1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA DUNIA LA WANASOKA WA MAJIANI NA BAYERN MUNICH YATWAA TAJI LAKE LA PILI MSIMU HUU

30 Mei 2005

Baada ya Ligi nyingi mashahuri za Ulaya kukamilisha msimu wa mwaka huu kwa finali ya kukata na shoka kati ya FC Liverpool na AC Milan ya Itali mjini Istanbul, mwishoni mwa wiki hii ilikua zamu ya finali ya vikombe vya shirikisho la dimba la kitaifa:

Katika uwanja wa Olimpik wa Berlin, mabingwa wapya wa Ujerumani Bayern Munich wsaliipikua tena Schalke 04 na kuizaba mabao 2:1 ili kutwaa kwa mara ya 5 vikombe vyote 2 vya nyumbani-Kombe la Ligi na Kombe la DFB –shirikisho la kabumbu la Ujerumani.Bao la ushindi la Munich lilikuja mnamo dakika ya 76 ya mchezo pale Mbosnia Salihhamidzic alipousindikiza mpira wavuni kutoka pasi maridadi aliopewa na Roy Makaay.

Kesho Bayern munich ina sababu nyengine ya kufurahia itakaposema ‘Auf Wiedersehen’ kwa heri kwa uwanja wa Olimpik wa Munich na kuhamia katika uwanja mpya utakaochezewa Kombe la dunia mwakani na bundesliga msimu mpya ALLIANZ ARENA.Uwanja huo mpya ulifunguliwa kwa mpambano wa kirafiki wa ma stadi wakongwe wa timu mbili za mtaani-bayern Munich na Munich 1860.Kesho lakini wataingia ma stadi kama Oliver kahn,Roy makaay,Michael ballaci kupambana na timu ya taifa ya Ujerumani kwa ufunguzi rasmi wa ALLIANZ ARENA.

Nchini Holland, kombe la shirikisho la dimba huko lilienda jana kwa PSV ei ndhoven walioizaba Willem II Tilburg mabao 4-0.Eindhoven imenyakua kwa mara ya kwanza vikombe vyote 2 nchini Holland.

Ama nchini Ureno Vitoria Setbul, imeizuwia Benefica Lisbon kutwaa mataji yote 2, kwani wao walilaza Benefica jana 2:1 na kutoroka na kombe hilo kwa mara ya tatu.Benefica walitwaa taji la ubingwa msimu huu.

Sambamba na Kombe la dunia mwakani hapa Ujerumani,Ujerumani itanandaa pia Kombe la dunia la wachezaji dimba mariani au vichochoroni mjini Berlin.Waziri wa michezo wa Ujerumani Otto Schily na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Jürgen Klinsmann wsalitangaza hapo jumamosi kile walichokiita, “Streetfootball world Festival”.Kombe hili la dunia la wacheza dimba mariani litaanza Juli mosi hadi 8 katika mtaa wa Berlin wa Kreuzberg.Ni sehemu ya mango wa utamaduni na sanaa wa seriali ya Ujerumani kwa ushirikiano na Radio Deutsche Welle katika mwaka wa Kombe la dunia.

Shirikisho la kabumbu la Afrika CAF lenye makamo makuu yake mjini Cairo, jana lilianza ukaguzi wa siku 2 wa viwanja vyote vitakavyochezewa finali ya Kombe la Africa la mataifa nchini Misri.Wajumbe wa Halmashauri-tendaji ya CAF walizuru jana viwanja vya dimba mjini Alexandria,Port sai dna Ismailia na leo wanazuru uwanja mkuu wa Taifa n aule wa kijeshi mjini Cairo.Timu 16 zitaania Kombe hilo kati ya Januari 20 na Februari 10 mwakani.

Ukaguzi sawa na huu utafanyika pia nchini Ghana kwa viwanja vitakavyochezewa Kombe la Africa la Mataifa 2008.Kinyan’ganyiro nchi gani ya africa itaanda kombe la dunia 2010 mwaka wa Kombe la kwanza la dunia barani Africa ni kati ya Algeria,Botswana,Libya,Morocco,Msumbiji na zambia ambazo zimeonesha hamu ya kuandaa Kombe hilo.

Katika kinyan’ganyiro cha Kombe la klabu bingwa barani Africa –Enyimba –mabingwa kutokla Nigeria watakumbana mwezi ujao na Ajax cape Town itakapoanza duru ijayo ya timu 6 .Enyimba inaania taji lake la 3 mfululizo.

Ajax Cape Town wanashiriki katika Kombe hili kwa mara ya kwanza .Hatahivyo, ni Al Ahly ya Misri ambayo yamkini ikawa pingamizi kubwa kwa Enyimba katika ndoto yake ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu.

Kaiser Chief-mabingwa wa africa Kusini wamefungiwa kushiriki katika mashindano ya vikombe vya Africa kwa kipindi cha miaka 3 baada ya kujitoa mwezi huu kucheza katika Kombe la Shirikisho la dimba la Africa.Kaizer chief ilitoa sababu ya kusheheni kwa kalenda yake ya mashindano nyumbani .

Ilikua icheze na Ismailia ya Misri.Kaizer Chief yenye makao yake mjini Johannesberg na mojawapo ya klabu tapiri kabisa barani Afrika, imepigwa pia faini ya dala 1.500.Kaizer Chief ilitawazwa mabingwa wa africa kusini wiki 2 nyuma na ingeiwakilisha nchi hiyo katika Kombe la klabu bingwa barani Africa msimu ujao pamoja na makamo-bingwa Orlando Pirates.

Majogoo wa Kenya walitamba mwishoni mwa wiki katika mashindano ya kila mwaka ya kimataifa ya riadha mjini Hangelo,Uholanzi:Kenya iliwika kuanzia mbio za mita 800 wanaume hadi mita 5000 wanawake:

Alex Kipchirchir alishinda mbio za mita 800 wanaume kwa muda wa dakika 1:46.90.

Isaac Songkok aliwaongoza wakenya wengine 2 kukumba nafasi zote 3 katika mbio za mita 3000 wakati Augustine Choge alimpiku muethiopia Tariku Bekele kutwaa ushindi wa mita 5000 ambamo mkenya mwengine Moses Mosop alimaliza watatu.

Kenya ilitamba pia katika mbio za mita 3000 kuruka viunzi ambamo Brimin Kipruto alinyakua ushindi akifuatwa na meknya mwengine Paul Koech nafasi ya pili.

Muethiopia bingwa wa Olimpik Kenenisa Bekele alitamba katika mita 10.000 akifuatwa na Abebe Negera pia wa Ethiopia.Ethiopia ilinyakua pia ushindi wambio za mita 1500 wanawake ambamo gelete Burika aliongoza.Kenya ilihetimisha ushindi wao huko Hangelo kwa kuwika katika masafa ya mita 5000 wanawake ambamo Isabella Ochichi alinyakua nafasi ya kwanza.

Mwishoe, mbio za magari huko Nuerbugering, hapa Ujerumani:

Bingwa wa dunia Michael Schumacher alishindwa tena kuwika jana alipomaliza 5 na gari lake la Ferrari.Ilibainika tena mara hii mbele ya mashabiki wa nyumbani Ujeruimani kuwa huu si mwaka wake.Mspain Fernando Alosno alitoroka na ushindi jana na hivyo anaendelea kuongoza katika mbio za magari za Formula one.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW