1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kombe la dunia la wanawake: Japan yazima ndoto za Norway

5 Agosti 2023

Japan imefaulu kudidimiza ndoto ya timu ya Norway katika michuano ya kombe la dunia kwa wanawake baada ya kupata ushindi wa mabao 3-1. Mchezo kati ya timu hizo mbili ulifanyika mjini Wellington, Australia.

Fußball-WM Frauen 2023 | Japan vs Norwegen
Picha: imago images/NurPhoto

Bao la kwanza la Japan lilipatikana baada ya mchezaji wa Norway Ingrid Engen kujifunga.  Goli la pili la Japan lilifungwa na Risa Shimizu katika dakika ya 50 na kunako dakika ya 81 Hinata Miyazawa akatia wavuni bao la tatu. Japan sasa imefuzu kuingia hatua ya robo fainali ambapo, itachuana na mshindi kati ya Marekani na Sweden ambaye atajulikana baada ya mechi yao hapo kesho Jumapili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW