Kombe la Dunia: Matumaini ya Rwanda yafifia
13 Oktoba 2025
Kocha wa timu ya taifa ya Rwanda, Adel Amrouche, amefichua kuwa aliumizwa sana na kushindwa kwa timu yake mbele ya mashabiki wa nyumbani akiwepo pia Rais wa Rwanda Paul Kagame. Amewataka mashabiki kutokata tamaa.
"Tumeumia sana, lakini huu siyo mwisho wa maisha, huu ni mpira wa miguu. Tunaweza kuiona Rwanda kwenye AFCON niamini."
Aidha Kocha Amrouche amewaasa wanyarwanda kuendelea kuipenda timu yao ya taifa na kupuuza tetesi zisizo na msingi, akisisitiza kuwa Amavubi (Timu ya taifa ya Rwanda) itaendelea kujengwa, iwe ni yeye au kocha au mwingine.
Kesho jumanne itacheza mechi yake ya mwisho ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026, ambapo imesafiri kuikabili Afrika Kusini.mjini Nelpsuuits.
Ushindi huo haukumaliza tu kampeni ya Rwanda bali pia umebadilisha mwelekeo wa kilele cha Kundi C. Benin sasa imekaa kileleni ikiwa na pointi 17, ikizidi Nigeria kwa pointi tatu kuelekea michezo ya mwisho ya makundi.
Muelekeo wa kundi C
Matokeo hayo pia ni pigo kubwa kwa matumaini ya Nigeria ya kufuzu. Licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Lesotho, Super Eagles sasa hawana udhibiti kamili wa hatima yao.
Katika mchezo mwingine muhimu wa kundi hilo, Zimbabwe na Afrika Kusini zilitoka sare baada ya pambano gumu, jambo lililozidi kufanya ushindani wa kufuzu kuwa mkali zaidi.
Kocha mkuu wa Benin Gernot Rohr, akiongea na vyombo vya habari amesema kwamba atakuwa na kibarua kesho na Super Eagles.
"Ingekuwa vyema zaidi kama Zimbabwe ingefunga bao, mambo yangekuwa mazuri, kwa sababu timu tatu zote zina nafasi ya kufuzu.
Tuna mechi ngumu zaidi. Ninawajua vizuri sana, si rahisi kushinda, hasa kwa kuwa Super Eagles wana nafasi ya kufuzu.
Kwa hiyo hii ni fainali leo ilikuwa kama nusu fainali, sasa tunakwenda kucheza fainali."
Kwa sasa, Rwanda inashika nafasi ya nne kwenye kundi C ikiwa na alama 11, huku Benin ikiongoza kwa alama 17, Afrika Kusini ikiwa ya pili kwa alama 15, na Nigeria ikiwa ya tatu kwa alama 14.