Kombe la Dunia: Partey anyimwa visa ya Canada
13 Juni 2026
Serikali ya Ghana imewasilisha rasmi malalamiko kwa Canada kufuatia uamuzi wa kukataa kumpatia visa kiungo wa timu ya taifa ya Ghana, Thomas Partey, kwa ajili ya Kombe la Dunia.
Partey, ambaye anakabiliwa na mashtaka ya ubakaji nchini Uingereza, hatashiriki mchezo wa kwanza wa Ghana dhidi ya Panama nchini Canada.
Waziri wa mambo ya nje wa Ghana Sam Okudzeto Ablakwa amesema uamuzi huo ni mkali kupita kiasi na hauna haki, ikisisitiza kuwa Partey ni mchezaji muhimu wa Black Stars.
Partey, mwenye miaka 32, amekana mashtaka saba ya ubakaji na moja la unyanyasaji wa kingono, na kesi yake imepangwa kusikilizwa mwaka ujao. Hata hivyo, FIFA imethibitisha kuwa hatasafiri na timu kwenda Canada kwa mechi yao ya kwanza dhidi ya Panama Juni 17, lakini atacheza mechi zinazofuata dhidi ya England na Croatia nchini Marekani.
Kwengineko kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amekosoa ongezeko la mechi katika soka la kimataifa, akionya kuwa wachezaji wako kwenye hatari kubwa ya kuchoka kupita kiasi. Ametaja kuongezeka kwa timu kwenye Kombe la Dunia na mashindano mengine kama mzigo unaoongezeka kwa wachezaji.