1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safu ya ulinzi ya Ujerumani kujaribiwa dhidi ya Morocco

Janek Speight Iddi Ssessanga
23 Julai 2023

Ujerumani inatinga Kombe la Dunia ikiwa katika hali mbaya, huku matatizo ya ulinzi yakiibuka katika mechi za kirafiki hivi karibuni. Tatizo huenda lisiwe kwenye mstari wa nyuma, hata hivyo, bali katika mkakati wa timu.

FIFA Frauen Fussball Weltmeisterschaft Australien 2023
Lina Magull anasema Ujerumani inahitaji bidii katika ulinzi ili kufungua nguvu ya mashambulizi.Picha: Eibner-Pressefoto/Memmler/IMAGO

Wakati Martina Voss-Tecklenburg akipania Ujerumani kusonga mbele vizuri kutoka hatua ya makundi ya Kombe la Dunia, suala moja la wazi linakikabili kikosi chake chenye vipaji: mashambulizi ya kujibu.

Ni udhaifu ambao ulibainika dhidi ya Vietnam na Zambia wakati wa kambi ya mazoezi ya kabla ya mashindano nchini Ujerumani, huku pande zote mbili zikitumia hamu ya Ujerumani kutawala michezo kwa kumiliki mpira na upasishaji wa juu.

Kipa wa Ujerumani Merle Frohms, hata hivyo, aliiambia DW wakati wa mazungumzo na wanahabari kwamba tatizo halisi halihusiani na safu ya ulinzi.

Soma pia: England wapata ushindi mwembamba dhidi ya Haiti

"Inategemea mchezo wetu wa mashambulizi na ukweli kwamba tunalinda sana na kuwaweka wapinzani chini ya shinikizo," alielezea.

"Hali hizo hazingetokea ikiwa tungekuwa na ulinzi zaidi. Lakini hiyo ni juu yetu kubaini hilo, kwa sababu ndivyo tunavyotaka kucheza."

Makosa ya kibinafsi uwanjani yalifichua udhaifu wa Ujerumani katika kipigo cha 3-2 dhidi ya Zambia, huku ukosefu wa nafasi ikiipa Vietnam wepesi katika ushindi wa 2-1.

Katika mechi yao ya kwanza ya Kundi H dhidi ya Morocco, watakuja dhidi ya timu yenye muundo wa hali ya juu ambao ni mahiri kiufundi na wana kasi ya haraka kwenye mawinga. Suluhisho zinahitajika haraka.

Morocco inaleta tishio lisilojulikana

Morocco hawako kwenye Kombe hili la Dunia ili kufurahia tu ushiriki wao wa kwanza; chini ya kocha Reynald Pedros wana imani na uwezo wao wa kushtukiza.

Ikiwa ni timu ambayo inapendelea kudhibiti mpira, Morocco huenda ikachukua mbinu ya tahadhari zaidi dhidi ya Ujerumani, kulingana na mwandishi wa habari wa Radio Mars Amine Birouk, ambaye anasema mawinga wenye kasi Fatima Tagnaout na Sakina Ouzraoui wanaweza kusababisha kitimtim kilichozoeleka kwa Ujerumani.

Morocco wamejipanga kwa ushiriki wao wa kwanza waKombe la Dunia.Picha: AFP/Getty Images

"Wanaweza kutumia mashambulizi ya kujibu kutengeneza nafasi nzuri," Birouk aliiambia DW. "Wana wachezaji wenye ufundi sana, wenye kasi katika mstari wa mbele, na pia mpangilio mzuri wa safu ya ulinzi.

"Ilikuwa ni wakati mzuri sana kupata kocha kama Pedros. Kuwa na kocha mwenye uzoefu kama huu, akiwapa uzoefu wasichana hawa, alibadilisha sura ya timu.

"Morocco haitaki tu matokeo mazuri, wanataka kutoa taswira nzuri ya soka la Afrika na Kiarabu."

Soma pia: Zambia yagaragazwa 5-0 na Japan

Iwapo Ujerumani itaepuka kurudiwa kwa masaibu yao dhidi ya Vietnam na Zambia, mchezo wao wa kushinikiza na wenye shinikizo lazima uinuke. Na mwanamke mmoja anaweza kuthibitisha kuwa muhimu kwa hilo.

Lina Magull muhimu kwa mchezo wa Ujerumani

Mpango wa mchezo wa Ujerumani huishi na kufa wakiwa na kasi yao juu ya uwanja na wakati huo unakwama, muundo wao unaweza kubatilishwa.

Lina Magull ni msanii mbunifu ambaye harakati zake, maono na kupita sehemu za ulinzi katika jukumu la Namabri 10 kunamfanya kuwa mmoja wa wachezaji hatari zaidi wa timu.

Kuvunja safu ngumu ya Morocco ni juu ya timu nzima, lakini inategemea sana fomu ya Magull pia. "Ni vigumu kupata suluhu au kutengeneza nafasi dhidi ya timu ambazo zinalenga zaidi ulinzi," alieleza.

"Nafasi ni ngumu sana na ni muhimu kuwa unasonga kila wakati, hata kama unahisi kuwa sio lazima wakati mwingine."

Magull anasisitiza umuhimu wa uhamaji mara nyingi. Uwezo wake wa kushuka chini zaidi na kuchukua mpira pia unaweza kutengeneza nafasi kwa wengine na mara nyingi huzunguka na viungo Lena Oberdorf na Sara Däbritz kuwachokoza wapinzani kutoka kwenye maeneo yao.

Soma pia: Uhispania yaanza vyema Kombe la Dunia la Wanawake

"Siku zote unajaribu kujitolea katika nafasi ngumu zaidi, pokea mipira na kisha ucheze pasi hiyo ya uhakika hadi katika nafasi ya tatu ya mwisho. Na jaribu kuwa kwenye eneo la hatari kwa wakati unaofaa kwa goli. Lakini kama timu lazima tuhakikishe kwamba tunajaribu kusonga mbele zaidi na kuelekeza umakini wetu kuelekea goli."

Lina Magull ni muhimu kwa taswira ya mpango wa mchezo wa Ujerumani.Picha: Murad Sezer/REUTERS

Pamoja na hayo, kasi ya juu ya Ujerumani na uwezo wa kushinda mpira wa pili ni muhimu kwa kikosi kinachofanya kazi vizuri. "Ni muhimu sana kwetu kuweza kusonga mbele," Magull alielezea.

"Ikiwa tutapoteza mpira huko juu, tuanze kukaba mara moja ili tuweze kurejea lango la wapinzani kwa kasi zaidi. Kazi ya ulinzi ni muhimu sana na wachezaji wote 11 wanatakiwa kufanya kazi kwa pamoja.

Soma pia: Bendera za jamii asilia kupepea kombe la dunia Australia na New Zealand

"Hilo linatufanya kuwa timu ya Ujerumani - kwamba tunafanya kazi kwa bidii kwa kujilinda ili kufanikiwa mwishowe."

Wachezaji wanaokosekana wanaifanya kazi ya Ujerumani kuwa ngumu

Kwa bahati mbaya, Magull na Ujerumani wana uwezekano mkubwa wa kukosa wachezaji wengine wawili nyota dhidi ya Morocco. Beki wa kati marshall Marina Hegering hajafanya mazoezi kwa urahisi kutokana na jeraha la kisigino, wakati Oberdorf amekuwa tu akishiriki majukumu mepesi kutokana na tatizo la paja.

Wote wawili ni hasara kubwa kwa Ujerumani, huku kukosekana kwa Oberdorf kukiathiri sana uwezo wa Magull wa kurandaranda na kuzingatia mchezo wake wa kushambulia.

Soma piaKombe la Dunia: Zambia itamkosa Chanda dimbani

"Yeye ni muhimu sana kwa sababu kwa Obi [Oberdorf] tuna mtu ambaye anasafisha kila kitu katika nafasi hiyo [ya kiungo wa ulinzi]," Magull aliiambia DW.

"Kujua kwamba yuko huko kunakupa usalama. Hiyo ni nzuri kwangu, kwa sababu ninaweza kuchukua hatua hatari zaidi ambapo ninaweza kupoteza mpira, nikijua kwamba Lena yuko nyuma yangu."

Uchambuzi wa michuano ya kombe la kandanda la wanawake

05:01

This browser does not support the video element.

Wakati Ujerumani ina wachezaji walio tayari kuchukua nafasi ya Sjoeke Nüsken kwa ajili ya ulinzi na chaguo kati ya Sydney Lohmann, Melanie Leupolz na Lena Lattwein katika safu ya kati, sio hali nzuri kwani wanajaribu kutatua masuala yao ya kimuundo. Jambo la uhakika ni kwamba Ujerumani haitabadilisha mpango wao wa mchezo.

"Ni kweli unajiandaa kwa kila mpinzani kiakili, lakini pia unazingatia mchezo wako mwenyewe," Felicitas Rauch alisema. "Siku zote nataka mpinzani wangu ajielekeze karibu nami."

Inastaajabisha, na ni jambo la kawaida miongoni mwa mataifa ya juu yaliyo na vipaji na nyenzo za kuunda miundo tata ya mbinu, hata hivyo inaweza kuwa kiburi wakati timu inapokataa kuzingatia mabadiliko ya mbinu.

Safu ya ulinzi ya Ujerumani iliachwa njiapanda mara nyingi sana katika mechi za kirafiki dhidi ya Zambia na Vietnam. Katika Kombe la Dunia, makosa kama haya yanaweza kuwa mabaya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW