1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoZambia

Kombe la Dunia: Zambia itamkosa Chanda dimbani

21 Julai 2023

Timu ya taifa ya soka ya wanawake ya Zambia imepata pigo kubwa siku moja kabla ya mechi yao ya kwanza ya michuano ya Kombe la Dunia kundi C dhidi ya Japan kesho Jumamosi.

OCEAUNZ Spielball FIFA Fußball Frauen-WM Australien und Neuseeland
Picha: Kolvenbach/IMAGO

Hii ni baada ya mshambuliaji wake muhimu Grace Chanda kuondolewa kwenye kikosi kinachoshiriki michuano hiyo.

Hili ni pigo la pili kwa kikosi cha kocha Bruce Mwape baada ya mlinda lango nambari moja Hazel Nali kuumia goti na nafasi yake kuchukuliwa na chipukizi Leticia Lungu.

Soma pia: Michuano ya Kombe la Dunia la wanawake yaanza rasmi

Daktari wa timu hiyo Faith Chibeza hakueleza zaidi sababu ya kutokuwepo kwa mshambuliaji huyo, lakini duru zimeliambia shirika la habari la Reuters kwamba amelazwa akipata matibabu.

Chanda ni nahodha wa zamani wa kikosi hicho na mchezaji muhimu aliyechangia kwa kiasi kikubwa kuliinua kwa haraka soka la kimataifa nchini humo katika miaka ya karibuni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW