Kombe la Dunia:Ujerumani yacharuka
14 Juni 2010Matangazo
Washambuliaji, Lukas Podolski na Miroslav Klose waliliona lango la Australia katika dakika 30 za kwanza.
Magoli mawili ya Ujerumani yaliongezwa katika kipindi cha pili cha mchezo, na Thomas Müller na Cacau.
Hata hivyo katika kipindi cha pili Australia ilibakiwa na wachezaji 10 baada ya Tim Cahill kuonyeshwa kadi nyekundu kwa sababu ya kucheza faulo.
Hapo awali Ghana iliibwaga Serbia kwa bao moja la penalti baada mchezaji wa Serbia kuunawa mpira ndani ya eneo nyeti katika dakika ya 86.
Kabla ya mechi hiyo Slovenia ijipatia ushindi wa kwanza katika mshindano ya kombe la dunia kwa kuifunga Algeria bao moja kwa bila.