1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KOMBE LA KLABU BINGWA AFRIKA LAANZA MSIMU MPYA.ZANZIBAR YAANZA VIBAYA KATIKA VIKOMBE VYA CAF NA GIOVANI ELBER ARUDI BUNDESLIGA:

31 Januari 2005

-Ligi mashuhuri barani Ulaya:

Kwa klabu zilizokua kileleni mwa Ligi za Ulaya, yalikua matokeo ya kufurahisha,lakini si kwa viongozi wa Ligi ya Ujerumani-Bundesliga:

Wakati FC Barcelona ya Spain na Juventus ya Itali zilitamba, Bayern munich iliondoka suluhu 0:0 na Berlin,lakini inaongoza sasa Bundesliga-Ligi ya Ujerumani kwa pointi 1 mbele ya schalke.

Uingereza,Ligi ilisita kuachia kinyan’ganyiro cha Kombe la FA na hakujakuwapo msangao mwengine-kwani madume wote viongozi wa Ligi-Chelsea,Arsenal na Manchester zote zilitia fora.

Ama katika Bundesliga, baada ya wiki nzima kuhanikiza kwa kisa cha rifu-mcheza kamari kwa kupanga matoko ya mechi alizochezesha Robert Hoyzer,Bundesliga ilirudi kutamba uwanjani.

Macho yalikodolewa mapambano 2:Bayern Munich dhidi ya Hertha Berlin na Schalke na Kaiserslauten.

Munich ikielekea kuitimua Berlin na kunyakua pointi zote 3,iliikuta berlin ikichachamaa na hasa kipindi cha kwanza.Ilikua kipindi cha pili ndipo Munich iliposhika usukani wa mchezo,lakini vishindo vyao vyote vilikua vya darini vilivyoishia sakafuni.

Mwishoe, Munich na Berlin ziligawana pointi baada ya kutoka suluhu 0:0.Sasa Munich inaongoza Bundesliga kwa pointi 38 kwa 37 za Schalke,kwani schalke ilichapwa mabao 2:0 na Kaiserslauten.Stuttgart wako nafasi ya tatu kwa pointi 34 baada ya kutandikwa mabao 4-2 nyumbani na Nüremberg.Bayer Leverkusen inanyatia nafasi ya 4 –wao waliizika Bochum kwa mabao 4-0.

Borussia Mönchengladbach, imemfun gisha mkataba mshambulizi maarufu wa Brazil aliekua akiichezea Bayern Munich, Giovani Elber.Elber amekuwa hadi sasa akiichezea Olympique Lyon ya Ufaransa.Amefunga sasa mkataba unaomalizika mwishoni mwa msimu huu 2005/06.

hivi sasa Elber ameumia baada ya kuvunjika goti lake la kulia August,mwaka jana.Glabach iko nafasi ya 15 katika orodha ya timu 18 za Bundesliga.

Katika Ligi ya Spain,FC Barcelona inaendelea kutamba:mwishoni mwa wiki ilikumta Sevilla 4-0-Mabao kutoka mkamerun Samuel Eto’0,Ronaldinho wa Brazil na Ludvic Giuly pamoja na bao lao wenyewe Sivilla yalitosha kuizika Sivilla.

Nchini Itali,mabingwa AC Milan walizidi kurudi nyuma kutoka kileleni baada ya kuzabwa bao 1:0 tena nyumbani na Bologna.Hili ni pigo la pili mfululizo kwa AC Milan na wameangukia sasa pointi 8 nyuma ya viongozi wa ligi-Juventus.

Katika ligi ya Ufaransa, mpambano wa Olympique Lyon na Bastia uliahirishwa,lkini Lille iliopo nafasi ya pili katika orodha ya Ligi,ilishindwa kuitumia nafasi hiyo na kuparamia kileleni.Ilimudu suluhu 0:0 na Caen.

KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:

Afrika imeanza msimu mpya wa Kombe lake la klabu bingwa,kwani sio tu msimu huu inamtafuta bingwa mpya bali pia muakilishi wake wa Kombe la Dunia la klabu bingwa litakaloaniwa nchini japn, Desemba, mwaka huu:

Firimbi ilipolia mwishoni mwa wiki,klabu ya wanajeshi ya Morocco FAR RABAT ndio iliotamba kabisa.

FAR iliitandika ACS Ksar ya Mauritania mabao 4:0.

Aviacao ya Angola,CAPS United ya Zimbabwe,Daring Club Motema Pembe ya kongo,Dophin ya Nigeria na Tusker ya Kenya zote zimeshindwa kwa alao mabao 3.Motema Pembe imeizaba Rayon Sports ya rwana mabao 3:0.T.P Mazembe ya J.K.ya Kongo ambayo rekodi yao ya miaka mingi ya kutwaa Kombe la Afrika mara 2 mfululizo ilisawazishwa msimu uliopita na Enyimba ya Nigeria,ilishinda 2:0 dhidi ya ASFA ya Burkina Faso.

Diaraf ya Senegal,Racing Club Bafoussam ya Kamerun na Simba ya Tanzania zilishindwa kutamba nyumbani na zimeondokea na ushindi si wa zaidi ya bao 1 tu.

Tusker ya Kenya iliifunidisha darsa KMKM –klabu ya kwanza ya Zanzibar kushiriki katika kinyan’ganyiro hiki cha kitita cha dala milioni 3.5 ilipowakomea mabao 4-1.

Mshambulizi wa Manchester City ya uingereza, Nicolas Anelka amefunga mkataba wa miaka 3 na nusu na Fenerbahce ya Uturuki.Mfaransa huyu aliejiunga na Manchester City, Julai 2002 kwa kitita cha dala milioni 18.77 amekuwa nje ya chaki ya uwanja tangu mapema mwaka huu kwa kuumia goti. Fenerbahce , inaongoza wakati huu Ligi ya Uturuki kwa pointo 4.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW